Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,142
- 5,877
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imewaachia huru wafanyakazi wawili wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Johnson Kato (57) na Gasper Kimaro (30) waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki, Wakili wa Serikali Aaron Titus alidai upande wa mashitaka umeamua kuwa hauna nia ya kuendelea na kesi hiyo kwa mujibu wa Kifungu cha Sheria cha 91 (1) kilichofanyiwa marejeo 2022. Hayo yalidaiwa mahakamani hapo jana wakati kesi hiyo ilipofikishwa kwa kutajwa.
“Washtakiwa mpo huru kuanzia sasa mpaka pale mahakama itakapoamua vinginevyo,” alisema Hakimu Nyaki. Kwa mujibu wa hati ya mashitaka Juni 30, 2023, Johson Kato na Gasper Kimaro wote wakiwa eneo la Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Ilala mkoani Dar es Salaam, kwa nia ya kutapeli, walijipatia fedha Sh milioni 390, Sh milioni 195 kila mmoja katika hundi mbili tofauti kutoka shirika lisilo la kiserikali la Community Development Trust Fund (CDTF) wakidai hundi hizo zilisainiwa na Henry Mgini, meneja wa shirika hilo.