Mhn...! kama una details, kwa nini usipeleke ushahidi kunako husika? wewe, lazima utakuwa ni mtu mbaya kuliko mchawi ambaye akikuua aanaua moja kwa moja, bora mchawi anakuchukua msukule, siku Mungu akikupitia, unarudi duniani. Lakini wewe ni muharibifu, unataka kushauri watu kuwa wewe ni mmoja wapo wa wafanyakazi wa Swissport, ambao kwa uelewa wangu ndio wanao fanya check in, kuwa mnachukua rushwa kutoka kwa abiria kwa kushirikiana na wafanya kazi wa mashirika ya ndege...!
Inawezekana ni kweli kitu hicho kipo..! siwezi kubisha kwani lisemwalo ..? lakini angalia usiwaharibie kitumbua cha watu wa swissport....!
lakini ole wao wote walongo..! umewahi kusikia mwizi anajitaja? na unasema bila kudai hongo maisha hayaendi, kwa nini msidai uongozi wa swissport uwaongezee mishahara badala ya kuwaonea wivu wenzenu walio weza kujikwamua kutoka swissport?
ninakerwa sana na tabia za watu walio kata tamaa ya kimaisha, na kisha kujawa na chuki za kibinafsi kwa wale wenzio wanao kwenda vizuri kimaisha, ni tabia chafu, na ya kukemewa, hilo pepo liwatoke wote wenye tabia hiyo, na badala ya ke wamuombe Mungu awasaidie na Mungu humsaidia yule mwenye bidii. Ongeza bidii hasa ya kisomo...!
Nimewahi pita airport mara nyingi kwenda na kurudi sehemu mbali mbali duniani, taratibu za mizigo ziko wazi kabisa na kama mtu amezidisha viwango basi huwa anapaswa kulipia, au la hasha hawezi basi anapunguza.
Nina ushahidi, nimetumia qatar mara nyingi tu tangu wameanza safari kupitia hapa Bongo huduma ni nzuri pale check in, na hata on board. na pia staff wao ni waelewa na hujali abiria.. hasa abiria anapokuwa na tatizo kama la kuzidisha mizigo... kwani imesha wahi kunitokea nikiwa delh kija dar, tena zaidi ya mara mbili. nilisaidiwa , wako reasonable. hivyo inakuwa ngumu kwangu mimi kuamini uyasemayao...!
Kama ndugu yetu una ushahidi basi tafadhali saidia taasiisi husika kwa kutoa taarifa natumaini huifadhi usiri wa mashahidi wa kujitolea, la kama huna huo ushahidi...? na ni majungu...? basi wewe jua umefuliaaaaaaaaaaaaaaaaaa!