Wafanyakazi wa Qatar Airways Punguzeni Baula (Rushwa) ya Mizigo Airport! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi wa Qatar Airways Punguzeni Baula (Rushwa) ya Mizigo Airport!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jul 12, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,180
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  wana jf kama inayojulikana kila mtu anakula madhbahuni mwake lakini kuna mambo ambayo inabidi uangalie jinsi ya kula usije kimbiza waumini ukaulizwa siku ya mwisho...hali hiyo imeanza kutokea kwa wafanyakzi wa qatar airways hapa airport ...si wao tu ni kwa kila airline company wanayofanyiwa check in kwa abiria kumwomba abiria alipe kiasi na hivyo kutopewa risiti....imekuwa kitu cha kawaida ila kwa hawa wenzetu imekuwa tabu hata kufanya nao kazi....wanaweza kukutumia ukachukua hata doller 1500 kwa siku siku ya mwisho unawapelekea wanakupa doller 25-40.....kibaya zaidi wameanza kudai pesa ambazo zinakaribia kabisa na bei halisi anayotakiwa kulipa abiria....ukiwaambia abiria analalamika wanajifanya kukaa pembeni na kutuachia mzigo mwisho wa siku tunaonekana wasaliti......kuna dada mmoja wa kipare anavaa miwani akishirkiana na mwenzake wa kipemba mnene kidogo alietokea SWISSPORT wanawasumbua sana abiria hata sie tunaofanya kazi ya kucheck in...tunawashauri kila mtu anakula baula lakini tusifanye kama ndio kichocheo cha kazi zetu yaani usipokutana na baula hakuna haja ya kufanya kazi...tukija kazini tuoende kazi kwanza vingine baadae....
  natumaini watajitahidi kjirekebisha ili na waumini wasiweze kukimbia kanisani....
   
 2. m

  msabato masalia Senior Member

  #2
  Jul 12, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wataje majina............acha kutembeza jungu.Hata ww inaelekea unakula hiyo kitu.Umedhurumiwa nini mkubwa?
   
 3. b

  bnhai JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Yaleyale na yeye anakula rushwa. Ukweli kuna tatizo kubwa saana katika viwanja vyetu vya ndege. Ukipita lazima uombwe cheti na jamaa wa uhamiaji hawakosi maswali yasiyo na kichwa wala miguu. Tatizo la airport Dar si ATCL tu bali ni mengi saana. I know the lady, she is graduate of UD, nasikitika kama na yeye ameingia kwa wala rushwa!
   
 4. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  What????

  Sijui unaeleza kitu gani hapo.
   
 5. W

  Wizard_of_odds New Member

  #5
  Jul 17, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhn...! kama una details, kwa nini usipeleke ushahidi kunako husika? wewe, lazima utakuwa ni mtu mbaya kuliko mchawi ambaye akikuua aanaua moja kwa moja, bora mchawi anakuchukua msukule, siku Mungu akikupitia, unarudi duniani. Lakini wewe ni muharibifu, unataka kushauri watu kuwa wewe ni mmoja wapo wa wafanyakazi wa Swissport, ambao kwa uelewa wangu ndio wanao fanya check in, kuwa mnachukua rushwa kutoka kwa abiria kwa kushirikiana na wafanya kazi wa mashirika ya ndege...!

  Inawezekana ni kweli kitu hicho kipo..! siwezi kubisha kwani lisemwalo ..? lakini angalia usiwaharibie kitumbua cha watu wa swissport....!

  lakini ole wao wote walongo..! umewahi kusikia mwizi anajitaja? na unasema bila kudai hongo maisha hayaendi, kwa nini msidai uongozi wa swissport uwaongezee mishahara badala ya kuwaonea wivu wenzenu walio weza kujikwamua kutoka swissport?

  ninakerwa sana na tabia za watu walio kata tamaa ya kimaisha, na kisha kujawa na chuki za kibinafsi kwa wale wenzio wanao kwenda vizuri kimaisha, ni tabia chafu, na ya kukemewa, hilo pepo liwatoke wote wenye tabia hiyo, na badala ya ke wamuombe Mungu awasaidie na Mungu humsaidia yule mwenye bidii. Ongeza bidii hasa ya kisomo...!

  Nimewahi pita airport mara nyingi kwenda na kurudi sehemu mbali mbali duniani, taratibu za mizigo ziko wazi kabisa na kama mtu amezidisha viwango basi huwa anapaswa kulipia, au la hasha hawezi basi anapunguza.

  Nina ushahidi, nimetumia qatar mara nyingi tu tangu wameanza safari kupitia hapa Bongo huduma ni nzuri pale check in, na hata on board. na pia staff wao ni waelewa na hujali abiria.. hasa abiria anapokuwa na tatizo kama la kuzidisha mizigo... kwani imesha wahi kunitokea nikiwa delh kija dar, tena zaidi ya mara mbili. nilisaidiwa , wako reasonable. hivyo inakuwa ngumu kwangu mimi kuamini uyasemayao...!


  Kama ndugu yetu una ushahidi basi tafadhali saidia taasiisi husika kwa kutoa taarifa natumaini huifadhi usiri wa mashahidi wa kujitolea, la kama huna huo ushahidi...? na ni majungu...? basi wewe jua umefuliaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
   
Loading...