Wafanyakazi wa NIDA na rushwa ndogo ndogo

livafan

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
2,925
5,528
Kusema ukweli hili zoezi la vitambulisho vya Taifa linaloendeshwa na NIDA Officers ni zuri sana lakini huduma za hawa watu ni mbovu sana na mpaka imefikia hatua binafsi nimeanza kuhisi harufu ya rushwa ndogo ndogo kama za (kujuana na hela ndogo ndogo za vocha) yawezekana hawa officers wa NIDA hudai kwa baadhi ya wananchi au sisi wananchi ni chanzo cha hili.

Kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu sasa nimekuwa nikifuatilia kitambulisho hiki cha Taifa bila mafanikio na hatua zote nimefuata, kuanzia Serikali za mitaa, zoezi la kujaza form, nikapiga pcha na hatimae kukusanya hizo form na mwisho wa siku nikaambiwa nisubiri kitambulisho baada ya wiki tatu hivi kitakuwa tayari hivyo nirudi kuchukua.

Lakini zoezi hili nimelifanya na sasa ni kama unaelekea mwezi wa tatu kuisha tangu nianze kufuatilia bila mafanikio, hii haimainishi ya kuwa sifati maelekezo no, nafuata lakini cha ajabu nazungushwa zungushwa tu na isitoshe nilijalribu kuongea na msimamizi wa kituo husika akaniambia kitambulisho kipo tayari, lakini nashindwa kuelewa kwanini sipewi.

Last week nilienda kituoni pia baada ya kuambiwa nirudi tulipoandika majina kwa ajili ya kutafutiwa hivyo vitambulisho, lakini nilipoenda nikakuta wanasoma majina ya siku ambayo nimeenda tuliyokuwa tumeandika hayakuwa yanafanyiwa kazi tena.

Ilinibidi niandike jina pia kwa ajili ya zoezi la kutafutiwa upya tena, cha ajibu Officer alikuwa anaandika hayo majina na kwa kutudharau tuliohudhuria apo akawa anapokea simu hapo hapo akisema wewe njoo sasa hivi naenda kutafuta kitambulisho chako, jiandae tu uje, alikuwa Officer mdada.

Officers wa NIDA kwa hili hamtendi haki, nahisi kwa hili sijakosea kuwasema, mjirekebishe na muweke mazingira mazuri ya wananchi kupata vitambulisho vyao, ni haki yao maana hela zinazotumika hapo ni kodi zao.
 
NIDA ni jipu lililoiva, linahitaji kutumbuliwa sasa...haiwezekani kila mtu analalamika kuhusu ucheleweshwaji wa vitambulisho vya taifa...mimi nimeamua kukiacha...kila siku nenda rudi...
 
Ilinibidi niandike jina pia kwa ajili ya zoezi la kutafutiwa upya tena, cha ajibu Officer alikuwa anaandika hayo majina na kwa kutudharau tuliohudhuria apo akawa anapokea simu hapo hapo akisema wewe njoo sasa hivi naenda kutafuta kitambulisho chako, jiandae tu uje, alikuwa Officer mdada.


Wasiojulikana wamejificha wapi kwenye hili
 
Ni moja wa utaratibu ovyo sana. Pale Kinondoni TTCL ndio wa ovyo kweli kweli. Kitambulisho kinachukua zaidi ya miezi 6. Kisha wanakwambia anza upya kujiandikisha.
 
Hata kwenye vitambulisho vya wapiga kura kulikua na rushwa.
Hajuna usimamizi serious hata kidogo.
 
Hapo ndipo utathibitisha ule usemi wa Rushwa ni adui wa haki
 
Back
Top Bottom