Mwana Kwetu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2011
- 652
- 562
Jana waziri wa mambo ya nchi za nje alisema wameanza kuwasaka wafanyakazi wa kigeni wanaofanya kazi zilezile watanzania wanaweza kuzifanya na hivyo kusababisha ongezeko la watu wasiokuwa na ajira.
Msianze mbali bali nendeni kwenye tours companies hapa Arusha. Makampuni mengi yanayomilikiwa na wageni hasa wahindi na wazungu(makaburu) wameajiri wafanyakazi wasio watanzania kwenye nafasi ambazo zinawezwa kufanywa na watanzania.
Kwa mfano kwenye kampuni ya Ker and Down na nyingine nyingi zimeajiri Tour Guides kutoka Africa kusini ambao ni makaburu wasiyoijua hata Tanzania. Wazungu hawa hubana kwenye magari yaliyobeba watalii kiti cha nyuma mwisho wakizuga kuwa nao ni watalii ili hali wako pale kuwaongoza wazungu. Wekeni mtego kwenye mageti ya kuingilia mbuga za wanyama mtawakamata wa kutosha. Tour guides wa kitanzania wako wengi na competent na wengi wa madereva wa kampuni za tours ni ma tour guides waliobobea lakini nafasi zao zinabanwa na hawa wazungu. Kitu cha kushangaza ni kuwa hata watalii wenyewe kutoka nje hawajisikii vizuri kuongozwa na tour guide wa kizungu.
Hawa ma tour guide wa kizungu wamekuwa wakichukua hata zile tips wanazostahili kupewa madereva wa Ki TZ kama asante kwa kuwafikisha watalii salama.
Naomba sana waziri wa mambo ya nchi za nje shirikianeni na madereva wa Tours wawape majina kwa siri ndio mtakwenda kugundua uozo wa kutisha .
Mawaziri wa utalii wa zamani akina Lazaro Nyalandu na Shamsa Mwangunga ndio walio lea hiyo tabia kwa kuwa walikuwa wakichukua kitu kidogo kutoka kwa wenye makampuni. Mawaziri hawa mara nyingi walionekana wakirandaranda kwenye ofisi na hata kulala hosteli za makampuni makubwa ya kitalii hasa yale ya kutoka nje ya nchi ambayo ndiyo yaliyokidhiri kwa kuwanyima watanzania ajira nzuri.
Naomba uhamiaji na wizara ya mambo ya ndani mfanye ufuatiliaji ili ajira zirudi kwa watanzania na tuweza kunufaika na rasilimali alizotupatia Mungu