Wafanyakazi wa Bandari mkae mguu sawa

Wafanyakazi wa Bandari mkae mguu sawa

Wafanyakazi wa bandari wajiandae kisaikolojia lolote laweza tokea lakini Mimi binafsi huu mkataba wa dp world ingekuwa sio baadhi ya terms za huu mkataba kuwa very controversial ningependa hao jamaa ndio wawe wana run Port operations kwa maana inaonesha wataleta ufanisi na kuleta uwajibikaji kutoka kwa wazawa .Kwa maana MTU mweusi bila mjaledi haendi ,na ndio maana baadhi ya taasisi za serikali ukienda upate huduma utajuta wafanyakazi wa serikali hawajali wataka huduma ,kibaya zaidi wana nyodo na zarau .
 
Na wajiandae kuhamia Mtwara, kigoma na bagamoyo kwa kauli ya katibu wa wizara alipoongea na wahariri wa vyombo vya habari " Bandari sio moja Tanzania,kama ya Dar es salaam itahitaji watu wachache basi tunazo zingine Tanzania"
Na uvuvi waache,sisi wabongo ni wavivu sana na kufanya kazi kwa mazoea..acha mwarabu aje atunyooshe
 
Na wajiandae kuhamia Mtwara, kigoma na bagamoyo kwa kauli ya karibu wa wizara alipoongea na wahariri wa vyombo vya habari " Bandari sio moja Tanzania,kama ya Dar es salaam itahitaji watu wachache basi tunazo zingine Tanzania"
Na uvuvi waache,sisi wabongo ni wavivu sana na kufanya kazi kwa mazoea..acha mwarabu aje atunyooshe
balaa
 
Kama wana uelewa basi ukifika muda wajitambue zaidi tutawasaidia kujitambua
 
Ukiangalia kwa jicho la tatu wanaopinga Hii issue ni wale wa maslahi Yao binafsi na si uzalendo wa kimaendeleo….na wanatumia nguvu na pesa nyingi kuwaaminisha wananchi ambao hawajui hata bandari kavu ni nini,yaani wengine hata bahari yenyewe hawaijui…

Embu fikiria Dp w angeleta mkataba wa kuendesha shirika la umeme kuna mwananchi ambae angekataa….mi mda huu tanesco wamekata umeme tena bila taarifa,huu si usnge
Kama DP World atafanya vizuri kwenye bandari,siyo mbaya akipewa na tanesco
 
Umeeleza kama unawasikitikia na unawapa tahadhari, yaani kama vile bandari (The Coast of Hope) imeanza kuanguka, ila haijafika chini, ikishafika, wataumia.

Lakini hakika uko sawa kabisa bandari inaenda na tulio wengi hatuumii kuhusu kwenda kwa mwekezaji bila kujali race yake.

Ila kinachouma wengi ni terms za mkataba kuwa za siri, na kwamba hadi leo hii hata Serikali haijasema kuwa ukifika wakati wa kusaini mkataba wenyewe, kama serikali wameamua kumpa mwekezaji miaka mingapi hata kama asingekuwa DP WORLD, bado maumivu yamekaa ki-fear of the unknowns.

Watanzania hawajaridhika na uwekezaji wa bandari, serikali isione aibu kuachana nao​

 
Pale bandarini kulikuwa na ufalme wao, kwa sasa kunapoelekea ule ufalme unaanguka rasmi unaingia ufalme mpya wa Dp world ambao utakuww unajitegemea pasipo kushurutishwa nani wa kumuajiri nani wa kumuacha maana ile sekta ni binafsi

Maana yake unatoka kuwa na kitambulisho cha uajiri wa serikali TPA ukibahatika kuajiriwa na DP basi unavaa gamba la sekta binafsi maana yake ww sio wa serikali tena , hapo ndio patam sasa, Maana wale wanatumia mitambo na Telnolojia kwa wingi kuliko wingi wa watu

Maswali mengi ni kwamba DP atakuwa anawalipaje wafanyakazi wake, je ni mfumo wa malipo ya kizungu au ndio ile mishahara ya wahindi 250,000 kwa mwezi, mawazo ni mengi sana

Hii inanifundishwa ukipata kitengo chochote iwe TRA au wapi kaa kwa Tahadhari sana maana mambo yanaweza kubadilika mda wowote
 
Back
Top Bottom