Wafanyakazi Guardian wamlilia na kumkumbuka Kamishina wa Kazi wa zamani Gabriel Malata

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,563
Huku bado wakiwa na majonzi ya kufiwa na mwajiri wao, Reginald Mengi aliyefariki dunia Dubai mwezi May mwaka huu, wafanyakazi wa The Guardian Limited wamesema uamuzi wa Rais John Magufuli kumteua Gabriel Malata kuwa Naibu Wakili Mkuu wa serikali mwa Septemba umewaathiri vibaya sana.

Malata ambaye hata Rais Magufuli alisikitika kumhamisha Ofisi ya waziri Mkuu na kumpeleka kwa Wakili Mkuu (Solicitor General) kwa madai kwamba alifanya vizuri kiwanyima vibali raia wa nje wasiostahili, alimnyima Meneja Unendeshaji wa TGL, raia wa India Bw Murugan Eswar mwezi Agosti mwaka huu,baada ya kukiuka masharti ya kibali chake kwani aliendelea kufanya kazi wakati kibali chake kimeisha.

Eswar ambaye kazi yake halisi ni manunuzi, alikamatwa na maafisa uhamiaji akiwa kazini TGL Mikocheni mwanzoni wa mwezi huu, lakini baadaye aliachiwa bila kufikishwa mahakamani na sasa karudi kazini akiwa amepata kibali kipya katika mazingira ya kutatanisha.

“Huyu bwana hana sifa zozote za kupata kibali cha kufanya kazi nchini lakini cha ajabu kapata kibali baada ya Malata kutoka ofisi ya serikali husika, pamoja na kwamba alikamatwa kwa kukiuka masharti, je kuna mazingira gani hapa kama siyo rushwa?” alihoji mmoja wa wafanyakazi hao aliyeomba kutotajwa jina.

Kampuni ya TGL imekuwa matatizo ya kuletewa wafanyakazi toka India wasio na utaalamu wowote na Mkurugenzi wa IPP Group, Zoeb Hassuji ambaye anatumia vibaya nafasi yake. Taarifa zinasema Hassuji akishirikiana na Kaimu Meneja Mkuu TGL, Srinivas Chintaluri na Mkuu wa Ulinzi, Ayoub Semvua kuwahonga watumishi wa serikali ili kupata vibali kwaajili ya wafanyakazi wasio na ujuzi wowote na ambao wanafanya kazi ambazo Watanzania wanaziweza.

Wahindi wengine waliopo TGL ni pamoja na Mkurugenzi wa Biashara, Ajay Goyal na Mkurugenzi wa Teknohama, Balaji Balasubramaniyan, ambao kazi zao zinafanywa na Watanzania Moez Kaderbhai na Avit Riwa ambaye mkataba wake ulisitishwa mwanzoni mwa mwaka huu kwa madai mshahara wake ni mkubwa. Bw.Riwa ambaye alikuwa pia Mhasibu Mkuu alikuwa anapokea mshahara mdogo ukilinganisha na Wahindi hao ambao pamoja na kulipiwa vibali pia wanalipiwa nyumba na wamepewa magari na madereva kwa gharama ya kampuni. Balaji ambaye haileweki hata ni kazi gani anafanya, amesababisha kusitishwa mkataba wa Dotto Makina ambaye ni Mtanzania ni kijana mtaaalamu wa IT.

Jambo la ajabu ni kwamba wakati Hassuji na wasaidizi wake wanafanya kila liwezekanalo kuwaleta Wahindi kufanya kazi TGL, kampuni imeendelea kufanya vibaya kibiashara kiasi kwamba wafanyakazi hawajalipwa mishahara kwa miezi miwili sasa, huku pesa nyingi ikitumika kuhonga maafisa wa serikali ili kupata vibali vya kazi na kuishi nchini.

Taarifa zinasema uongozi wa TGL kwa kushirikiana na Hassuji umelipa zaidi ya 20m/- kwaajili ya kibali cha Eswar na rushwa ili asifikishwa mahakamani wala kupigwa PI na uhamiaji baada ya kukiuka masharti ya kibali chake.

Mwisho.
 
Hiyo kampuni ikibakia mikononi mwa waswaili inakufa sasaiv tunaizika waacheni wahindi walikuwepo tang enzi za mzee Mengi hamjiuliz nawambieni vijana wa kiswahili majungu mengi hakuna kazi waacheni wahindi na wachina wawakanyage hutaki hachs kazi. Natafta wahindi wanisaidie jaman kuwakanyaga vijana wa kiswaili mm nawachukia sanaa vijana wa kiswaili kazj majungu tu
 
Hiyo kampuni ikibakia mikononi mwa waswaili inakufa sasaiv tunaizika waacheni wahindi walikuwepo tang enzi za mzee Mengi hamjiuliz nawambieni vijana wa kiswahili majungu mengi hakuna kazi waacheni wahindi na wachina wawakanyage hutaki hachs kazi. Natafta wahindi wanisaidie jaman kuwakanyaga vijana wa kiswaili mm nawachukia sanaa vijana wa kiswaili kazj majungu tu
Utakua mhindi mweusi wewe si bure
 
Back
Top Bottom