Mkuu majebere, umesema pesa hiyo ya kodi inahitajika sana na serikali ya Sisiem, kwa kuwa uchaguzi umekaribia, unataka kutuambia mnazihitaji sana pesa hizo ili mkanunulie fulana, khanga na kofia, ili muwahonge wananchi, na kuwafanya wapiga kura hao kuwa mabango yenu ya matangazo, kwa kuvalia sare hizo za chama chenu cha magamba?Waailete za kuleta, janja ya kutaka kwepa kodi hakuna sasa. Hela inahitajika, uchaguzi umekaribia
Kulipa kodi siyo tatizo, tatizo ni hizo kodi zinaliwa na wachache. Kwanza ccm iondoke ndiyo watu watakuwa na imani na kulipa kodiWafanyabiashara leo tarehe 27 wamegoma nchi nzima kwa madai ya kutaka kukutana na serikali TRA kujadiliana njia bora zaidi ya kulipa kodi tofauti na ilivyo sasa ambapo wafanyabiashara wanakandamizwa na sheria mpya ya kodi ilipitishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Anzeni ushawishi "lobbying" ili ifanyiwe marekebisho. Lakini lendila biashara ya kuuza kuku zilizookwa pale Nairobi na Mtu mwenye duka Kariako nani mfanya biashara mkubwa? kwa nini yule muuza kuku na kababu pale Nairobi atumia machine ya kodi ya kutolea risiti ninyi wenye maduka ya Jumla kariakoo msitumie machine za TRA?
Wafanyabiashara leo tarehe 27 wamegoma nchi nzima kwa madai ya kutaka kukutana na serikali TRA kujadiliana njia bora zaidi ya kulipa kodi tofauti na ilivyo sasa ambapo wafanyabiashara wanakandamizwa na sheria mpya ya kodi ilipitishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ss wafanyabiashara nia yetu ni kukaa na serekali meza moja tupange njia nzuri zaidi ya ulipaji kodi wa haki sasa kuna ubaya gani kama nia ni kukaa na wafanyakazi wetu tuliyowajiri wenyewe
Waailete za kuleta, janja ya kutaka kwepa kodi hakuna sasa. Hela inahitajika, uchaguzi umekaribia
Huwezi kuelewa jambo hili linawaumizaje hao wanaodai haki yao hadi uwe mfanyabiashara na unayelipa kodi.
Ndio utawaelewa hao watu, kinyume na hapo utakuwa unaongea tu kufurahisha nafsi.
Kumbe wanaogoma ni wachuuzi maana hata kina Mengi, Manji, Barharesa, Mimi ni wafanyabishara lakini hatuko kwenye mgomo. Manaposema wafanyabishara wote wamegoma mnakuwa hamjatenda haki kwa wengineo ambao hatuna tatizo na mashine za TRA kwa sababu hatuna cha kuficha.
Tukana uwezavyo lakini kodi ni lazima kwa maendeleo na ustawi wa taifa letu la Tanzania. Ni suala la wakati tuu lazima sheria za Nchi zifuatwe. Umoja wenu ungekuwa na maana kama mngepenyeza ushawishi wakati ule sheria ya EFD Machine inatungwa lakini siyo sasa
Wasiotaka kununua mashine za efd wanyang'anywe leseni za biashara. Kodi ni lazima ilipwe kutokana na mapato na efd ndiyo itaonyesha mapato halisi. Wafanyabiashara ni wakwepaji wakubwa wa kodi. Wafanyakazi ndiyo wanalipa kodi kulingana na mapato yao. Tra iwaorodhesha wote waliogoma na kuhakikisha wanafutiwa leseni zao za biashara.
Efd ni tatizo kuna jamaa yangu anatumia hiyo mashine ameenda kukadiliwa kaambiwa alipe Mara 2 ya mwakajana. Alipohoji kwa nn wasitumie taarifa za efd wakamwambia hawaamini kama taarifa zimeingizwa sahihi. Hakuna umuhimu wa kununua mashine hizo