ISLETS
JF-Expert Member
- Dec 29, 2012
- 8,121
- 5,332
Salamu kwa wafanyabishara wote, aluta continua.....
Kuna ishu moja binafsi imekuwa kero sana kwangu naona niiseme tu. Maeneo mengi ya biashara au ofisi za kazi mfano saluni, hotel/migahawa, dukani, nk kuna tatizo kubwa la kujazana watu wasio wateja, unakuta ni washkaji zako tu wamekaa kihasara harasa, hii kitu inakera sana na wakati mwingine wateja huwa tunakwazika.
Mfano unaingia barber shop, unakuta watu kama 10 wamekaa, kati ya hao wateja ni watatu tu, wengine wote wamekuja labda kuona mpira, hii huwa mnaona ni sawa?
Mtu anaweza kudhani kuna foleni akaaga akaondoka. Au akakaa tu ila asifurahie ile hali. Najua si mimi tu ninayekereka na hii hali.
Au, unakuta ni hotelini, umekula umemaliza, unapita counter kulipa unakuta mhudumu yuko bize na stori na mtu mwingine na wanachoongea ni nje ya kazi kabisa, wakati huo kapokea hela unasubiri chenji, hivi huwa hamgundui kuwa ni kero!!
Unapita dukani kununua kitu, unakuta watu wamekaa dukani, hawanunui kitu, ni stori tu na mwenye duka, au wanachungulia mpira kwenye Tv ya dukani. Mteja anayehitahi utulivu hawezi ingia duka kama hilo, atapita tu kama hajaliona vile.
Mifano hai ni mingi, kifupi mjue tu kuwa huwa mnafukuza wateja. Sio kila mtu anapenda misongamano na makelele. Ni vyema kama una ndugu au mshkaji kaja kupiga stori eneo la kazi, mchane makavu kuwa upo kazini, utamtafuta baada ya kazi muongee vizuri.
Na wale mnaopenda kujazana kwenye ofisi za watu kiharasa hasara, kupiga zogo au kuona mpira, kanunueni ving'amuzi vyenu au muende vibanda umiza, sio kuharibu biashara za watu.
Ni hayo tu.
Hasta la vista
Sent using Jamii Forums mobile app