Hakuna timu kubwa yeyote duniani isiyo na wadhamini. Vinginevyo, timu hishia hapo hapo pindi masuala ya kifedha yanapolegalega. Mfano wa timu zenye matatizo ya kiufadhili ni Portsmouth ya Uingereza ambayo sasa hivi iko mkiani kwenye msimamo wa ligi. Ilikosa hata fedha za kulipa mshahara wa wachezaji.
Hivyo, kwa vyovyote vile ili timu iwe imara kushindana lazima iwe na uwezo wa kujiendesha kifedha kwa maana ya kuwa na chanzo imara cha mapato ikiwa ni pamoja na wafadhili. Mimi mnazi wa Manutd kwa mfano wa wafadhili wake ni AIG, Nike, Audi, Hi Seoul, Kumho Tires n.k. Hiyo in mifano kwa manutd pekee, hivyo iwe Barcelona, Arsenal, Chease na timu zote lazima zina wafadhili wao wa kuaminika.
Hivyo Yanga siyo vibaya kuendelea kumuomba Manji aendelee kufadhili timu kama hawajapata wafadhili wengine wa kuaminika maana ni muhimu kwa mafanikio ya club.