Manipulators, ukijua namna ya kuishi na hawa watu hautateseka sana.
Mtu unaishi nae ghetto moja ila sasa unaona kabisa anayoyafanya ni mambo ya hovyo, uwezo wa kumfukuza unao ila kila ukitaka kumfukuza unashindwa ni kama anakusoma mapema sana anakutengenezea mazingira mapema sana siku ukitaka kumfukuza unaona kabisa unakosea unaamua kuendelea kukumbatia bomu kwa upendo mkuu..
Kuna kipindi nilikuja kugundua kuwa ukienda ugenini ili ukae pale kwa muda mrefu sana kwanza mtu wa kujenga uhusiano mzuri ni mtoto au watoto wa pale kisha mama yao kwa upande wa baba mwenye nyumba huyo hata mkiwa hamuelewani ni sawa tu utakaa muda unao utaka wewe iwapo una maelewano mazuri na watoto na mama mwenye nyumba, hii ni aina ya manipulation.
Kuna msichana niliwahi kumpenda sana lakini kadri siku zilivyokuwa zinaenda nikawa naona kabisa ameanza kuingiwa na tamaa nikaanza kutengeneza mazingira ya kunikosea yaani kitu kidogo tu ila akisema anifokee mimi simjibu halafu baadae anakuja ananiomba msamaha yeye mwenyewe na wakkati hana kosa.
Na hawa manipulators wengi ndio huwa ni playboys na playgirls.. Yaani anaplay victim kudai kuwa anakupenda mpaka unahisi huyu sasa nikisema nimuache anajiua halafu ukimuacha ana moveon..
Na uwezo wa kufanya haya yote nadhani huwa ni uwezo wa kuzaliwa nao sio kila mtu anaweza kufanya hivyo.