Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
Kumekuwapo vikao vya wadau wa jengo la Ubungo Plaza, baada ya Wahindi wanaoendesha hoteli hiyo kutofautiana na menejimenti ya jengo la Ubungo Plaza.
Tayari wadau wa Ubungo Plaza, Shirika la Bima (NIC), NSSF na PSPF wamekutana kujadili hatima ya wamiliki hao ambao wanadaiwa kuingia katika jengo hilo wakiwa na nia ya kufilisi Ubungo Plaza Limited kwa kuifungulia kesi za kisanii.
Kesi moja wapo walifungua wakidai kwamba bawaba za milango ya jengo zilikuwa mbovu badala ya kushirikiana na menejimenti kurekebisha kama kweli zilikuwa na matatizo. Kama kawaida wakacheza na mahakama za chini wakashinda kesi lakini Ubungo Plaza wakakata rufani. Wakati rufani imekatwa wakaenda mahakamani kutaka kukazia hukumu walipwe Shilingi Bilioni sita (6bn/-) kama fidia, lakini wakaambiwa kuna hukumu.
Baada ya mahakama kusikiliza hukumu imebainika kwamba hawakuwa na hoja na hivyo Ubungo Plaza Limited wakashinda kesi na ndio sasa wameshituka na kupanga kuwatimua.
My take:
Majengo ya mifuko ya pensheni lazima waendeshaji wawe makini na matajiri maana inawezekana kabisa ndio michezo inayoendelea kama menejimenti haitakuwa makini kama ilivyokuwa kwa Ubungo Plaza. Wengine huwa wanakula na hao matajiri na kuachia tu mifuko inalipa mabilioni katika kesi za aina hii. Kuna kesi nyingi mahakamani zinazohusu taasisi za umma na wanasheria wanacheza na wahuni wachache na kusababisha fedha za wafanyakazi na za umma kupotea. Tusaidiane kufichua hizi kesi kadiri tunavyoweza ili tupige kelele na kusaidia kuokoa fedha zetu.