Wadau wa michezo embu tujadili sakata la udhamini wa GSM katika ligi yetu

Smt016

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
2,272
2,994
Nimejaribu kusoma maoni mbali mbali humu zingine zikiwa za wana yanga wengine zikiwa za upande wa simba wakijibizana na pia wengine kukosoa juu ya hatua ya TFF kusaini mkataba na GSM. Mkataba wa GSM na TFF umeleta taharuki kubwa sana kwasasa ila ifuatayo ni maoni yangu.

Cha kwanza kwa upande sijaona tatizo la GSM kudhamini ligi yetu maana inakuwa ni sehemu ya mapato kwa vilabu vyetu, lakini nimesikitika kwa aina ya namna uswahili ulivyotumika kuliko kutumia akili na usomi. Kwanini nasema uswahili;

GSM inatakiwa iwe taasisi inayojitegemea isiyofungamana na upande wa taasisi ya Yanga katika kiutendaji na kiutawala lakini cha ajabu ni kwamba huwezi kutenganisha Yanga na GSM. Kwenye mambo ya kiundeshaji wa timu ya Yanga bwana Hersi Said kutoka GSM haumkosi. Kuna kamati ziliundwa na Mshindo Msolwa ambapo Hersi Said pia yupo.
Kosa la kwanza ni hilo la mdhamini wa ligi anapaswa asiwe anafungamana na timu fulani lakini GSM na Yanga ni kama baba na mtoto kiasi kwamba kiongozi kutoka GSM anatamka kuwa Yanga ikikosa ubingwa waulizwe wao.

Kosa la pili ni kitendo cha viongozi wa Yanga kuonekana katika makabidhiano ya mkataba, utafikiri Yanga ni miongoni mwa taasisi inayodhamini ligi pamoja na GSM. Na hili limetokea kwasababu kama niliyosema juu kwamba kuna muingiliano wa kiutendaji baina ya watu kutoka yanga na GSM. Hapo ukichukua na tambo za msemaji wa Yanga kuhusu huo udhamini na kuwakera upande wa Simba.

Hayo ni mapungufu nayoyaona mimi, kuna hoja zinatolewa na upande wa Simba kwamba kwanini kwenye huo mkataba timu hazijashitikishwa. Hii hoja inaweza kuwa sahihi endapo tu mikataba iliyoingia TFF baina ya Azam, TBC, na NBC zimezishirikisha klabu zinazoshiriki ligi kuu.

Kama mikataba yote waliosainia TFF na hao wadhamini wengine waliotangulia haikuvishirikisha timu zinazohusika, basi hata hili la GSM na TFF kutoshirikisha vilabu ni sahihi ni imetendeka sawa sawa na mikataba mengineo.

Karibuni wana jamvi kwa maoni kuhusu hili ila naomba tusijikite kwenye ushabiki wa usimba na uyanga.
 
Huko uwanjani tayari. GSM amelambishwa chini. Hakuna bango hata moja lake.
Nimejaribu kusoma maoni mbali mbali humu zingine zikiwa za wana yanga wengine zikiwa za upande wa simba wakijibizana na pia wengine kukosoa juu ya hatua ya TFF kusaini mkataba na GSM. Mkataba wa GSM na TFF umeleta taharuki kubwa sana kwasasa ila ifuatayo ni maoni yangu...
 
TFF kweli wana bahatisha mambo na wenyewe hawana msimamo nimeskia wameenda kuyatoa mabango ya gsm uwanjani baada ya simba kupiga mkwara kwamba hawata ingiza timu kama mabango ya gsm hayata tolewa.
 
TFF kweli wana bahatisha mambo na wenyewe hawana msimamo nimeskia wameenda kuyatoa mabango ya gsm uwanjani baada ya simba kupiga mkwara kwamba hawata ingiza timu kama mabango ya gsm hayata tolewa.

Umeiona ile barua kutoka CAF,tena wamepigwa mkwala Board ya Ligi na siyo TFF maana ndiyo hasa walipaswa kuhusika na mikataba ya aina hiyo.Lakini kwa ujuaji wa TFF wakabeba jukumu lisilowahusu,nadhani sasa nidhamu itakuwepo na kama kweli GSM anataka kuwekeza kwa ligi,basi taratibu zote zifuatwe kwa uwazi kupitia Boar ya Ligi na siyo TFF.
 
Tff pale Nadhani imejaa matahira,

Unasaini mkataba ambao hakuna timu inayojua itafaidikaje na huo mkataba. Wakati wanasaini nilidhani udhamini ni kwa timu ya taifa ndo badae nasikia ni kwa ajili ya ligi na mbaya zaidi ikatolewa barua hakuna wa kujadili mkataba isipokuwa tff na gsm, ujinga wa wa sgr huu.

Ule mkataba hauwezi kuja kufanya kazi bila vilabu vyote kushirikishwa kupitia Bodi ya Ligi.
 
Back
Top Bottom