Angalizo, mtoto ukimpeleka Diploma akitokea form four, mpeleke vyuo vyenye diploma 100%.
Kama utampeleka vyuo vikuu ambavyo pia siku hizi vina course nyingi za diploma, jiandae kwa lolote.
Watoto wanaosoma Diploma kwenye vyuo vikuu wanateseka sana kwasababu ya interaction kubwa na wanafunzi wa degree na masters.
Wanaishia kuwa vyakula vya hawa wenye maboom Yao.
Halafu mtoto wa form four akili haijapevuka vizuri kupambanua mambo au kuresist vishawishi vya makundi Rika.
Kwa hiyo kupanga ni kuchangia ndugu wazazi.