Wadau natafuta soko la mihogo mibichi

Wadau natafuta soko la mihogo mibichi

Shuku_

Senior Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
191
Reaction score
273
Habari zenu wana jf, Bila kuchelewa twende kwenye mada kama kichwa kinavyo jieleza natafuta soko la mihogo mibichi, Huku nilipo Morogoro Turiani mihogo mibichi inapatikana kwa wingi tu nna mpango wa kuinunua kwa mkulima na kuisafirisha tatizo lipo kwa upande wangu sijui pakupeleka.

Natanguliza shukrani kwa msaada wenu wadau.
 
Miogo ivune Kisha toa tope/mchanga bila kuimenya vile vile na magamba ikatekate kilo moja,ntakupa 190 Mia na tisini.nachukuwa yotee. Hapa Dar,
 
Kiongozi huku tunanunua kwa viroba vya Kg 25 labda nikuuzie kwa kiroba.
 
unataka uchukue kwa kihasi gani nikaulizie soko kwa madalali sokoni....ni partnership.
Kwasasa uwezo wangu wa kununua huku ni viroba 10 vya kg 25 endapo mtaji ukiongezeka nataka kubeba kwenye Canter au Fuso
 
Soko lipo mkuranga dsm wanaunua kwa k ilo.
Shs. 90 kwa kilo.
na wanapenda mbegu ya kiroba ila nadhani wana unua yote. Ukipeleka mpunga hapo
 
kila kiroba shingapi? Vema tukianza na viroba 100
Natumia elfu 13 kununulia kwa kila kiroba, Mkulima ananiuzia elfu 10, Kukisafirisha kutoka shamba hadi barabani ni elfu 3 kwaiyo jumla ni elfu 13 kwa kiroba kimoja.
 
Soko lipo mkuranga dsm wanaunua kwa k ilo.
Shs. 90 kwa kilo.
na wanapenda mbegu ya kiroba ila nadhani wana unua yote. Ukipeleka mpunga hapo
Mkuu huko mkuranga itakuwa ni chaka sana maana mi kiroba nanunua kwa elfu 13 ukipiga hesaba haraka haraka hicho kiroba cha kg 25 ukikipima kwa makadirio inaweza kufika kg 40 au 50 kwaiyo ukizidisha Kg 50 × 90 tsh = 4500. Siwezi kufanya hiyo biashara kichaa.... Over... Over... 🔊🔊🔊
 
Kilimo ambacho hakina soko linaloeleweka! Mie niliongea na wadau before hasa Tantrade na kuna chama cha kuunganisha masoko ya mazao wapo Mkuranga pale.

Walinipa moyo soko lipo kubwa sana nishindwe mimi.

Mihogo ilipokomaa, hawana soko tena!! Niita canter za Buguruni wakabeba mihogo yao nami nikabaki na hasara yangu!

Nenda soko la Stereo Temeke na Buguruni hapa Dar japo walaliani mno! All the best Dude
 
Soko lingine la mhogo mbich

sawa hilo ni soko la wa kule kule .

tuambie huko shina moja linafikia kg ngapi ?
 
Kilimo ambacho hakina soko linaloeleweka! Mie niliongea na wadau before hasa Tantrade na kuna chama cha kuunganisha masoko ya mazao wapo Mkuranga pale.
Walinipa moyo soko lipo kubwa sana nishindwe mimi.
Mihogo ilipokomaa, hawana soko tena!! Niita canter za Buguruni wakabeba mihogo yao nami nikabaki na hasara yangu!
Nenda soko la Stereo Temeke na Buguruni hapa Dar japo walaliani mno! All the best Dude
Pole sana kwa majanga hayo na Asante mkuu kwa kunifumbua macho ila wadau wengi humu wanasema huko sokoni wananunua kwa kg mdau mmoja kasema wananunua tsh 90 na mwingine amesema ananunua tsh 190 nami nkipiga hesabu hailipi hata nusu ya gharama ya manunuzi.
 
kwanini usikaushe,ukasaga unga na kupack?,ukaweka packaging nzuri,ukauza supermarket unga wa muhogo?
Mkuu kuhusu hilo cjui A B wala C au labda nimpate mtu anayefanya hivyo usemavyo ili nijue A mpaka Z kupitia yeye.
 
Habari zenu wana jf, Bila kuchelewa twende kwenye mada kama kichwa kinavyo jieleza natafuta soko la mihogo mibichi, Huku nilipo Morogoro Turiani mihogo mibichi inapatikana kwa wingi tu nna mpango wa kuinunua kwa mkulima na kuisafirisha tatizo lipo kwa upande wangu sijui pakupeleka.

Natanguliza shukrani kwa msaada wenu wadau.
Mkuu kwa Kwanza Ni Aina gani ??? Kisha nakushauri fuatilia masoko na Kama una mtu aende moja kwa moja sokoni na ajue Ni Aina ipi ya mhogo iko sokoni ndio upeleke

Humu hutopata jibu lilo na uhakika asilimia Mia
 
Back
Top Bottom