Wadau na Jukwaa muhimu zaidi ndani ya JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadau na Jukwaa muhimu zaidi ndani ya JF

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by firstcollina, Jun 18, 2010.

 1. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ama kweli wahenga walisema kwenye Miti hakuna wajenzi, sasa ndio naanza kutambua kuwa waliona mbali, nasikitika sana kuona waliondoka bila kutuachia namba za simu wala sanduku la posta huenda tungali wauliza mawili matatu nakufaidi zaidi.

  Nalazimika useyasema hayo mara baada ya kupata wazo la kufanya kautafiti kafupi hapahapa ndani ya JF hasa katika Jukwaa la Elimu (Education Forum). NInachojua ni kwamba founders wa JF waliona mbali sana na pia walikuwa na umakini na Ubora mkubwa sana katika kutengeneza hii Forum (JF) haya unaweza kuyaona katika muundo mzima na utaratibu wake katika shughuli za kila siku za JF. Kimbembe kinakuja pale members wanapo anza shughuli zao ndani JF.

  Ni ukweli kila mtu yupo huru katika kuchangia maada yoyote ile katika jukwaa analoona linamvutia, hilo mimi sina tatizo nayo, tatizo linakuja pale panapohitaji kupewa kipaumbele.

  Ikumbukwe kuwa, katika nchi inayohitaji kuendelea kama Tanzani, ni jambo lisio na kificho kwamba Elimu ni mojawapo ya jambo muhimu kabisa kuzingatiwa hasa ukichukulia kuwa Ujinga ni moja wapo ya adui mkubwa wa taifa letu na Elimu ndio tiba sahihi ya maradhi haya ya Ujinga. Kwa kuzingatia hayo ndipo nilipopata wazo la kuangalia mitazamo ya watu katika Taifa juu ya umakini na Juhudi za makusudi za mmoja mmoja katika kupambana na adui huyu Ujinga, kwa kuanza ni kaanza ndani kwangu (ndani ya JF the Home of Great Thinkers) mmh, nakuambia...! Kimbembe...!!

  Nilichokiona ni kitu rahisi sana lakini kikanipa mashaka na ndipo nilipoona umuhimu wa kuandika post hii ili tupate kuchangia na yeyote yule atakaye pata nafasi au bahati ya ku-view hii post.
  Nadharia
  Kinadharia, katika hali tete kama tuliyonayo ndani ya nchi yetu teule ya Tanzania, ili tupate kujikwamua ilikuwa ni lazima kuwekeza katika Elimu, jambo ambalo JF founders waliliona na katika hatua za makusudi kabisa za kulikabili ndipo walipoanzisha jukwaa la Elimu (Education Forum)

  Wajibu na Kujitambua
  Ilikuwa ni wajibu wa kila mtu anayependa mabadilko ya kweli kuchukua hatua za makusudi za kubambana na adui huyu Ujinga kama ambavyo hayati baba wa taifa Mwl. J.K. Nyerere alivyo chukua hatua na kulitangaza kuwa Ujinga ni moja ya janga la kitaifa. Hivyo katika hali ya kawaida kwa watu makini na wenye ufahamu na nia thabiti ya kulitokaomeza hili lazima kungekuwepo na juhudi za hapa na pale katika kuhakikisha tunajaribu kama sio tunafanikiwa katika kulitokomeza hili. Hivyo kutokana na hayo yote utakubaliana na mimi kwamba basi jukwaa hili la Elimu ndio jukwaa kuu kuliko yote kutokana na umuhimu mkubwa na nafasi lililonalo katika kuisaidia Tanzania katika kumtokomeza adui huyu Ujinga

  Observations
  Ukifungua jukwaa la Elimu utakuta kuna wastani wa thread 2 mpaka 3 katika wiki nzima, mbali na hayo katika kila thread kuna wastani wa watu 3 mpaka 5 kuichangia thread husika katika bases ya wiki, pia kuna wastani wa watu 37 mpaka 64 wanao-view thread husika katika wiki nzima. Ulinganifu mwingine waweza fanyika katika wastani huu hapa chini mpaka usiku wa jana 17/06/2010

  Forum Post Celebrities Forum 30,999 Mahusiano na Mapenzi 96,025 Habari na Hoja 117,353 mchanganyiko Elimu 12,175

  Kinacho nisumbua mwenzenu hivi kweli hii ni jamii ya watu makini kwelikweli?????? Are we really serious??
  Please advice......
   
 2. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  I'm not even sure if you as well you are SERIOUS!
   
 3. Kitumbo

  Kitumbo JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 547
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Labda kwa vile watu wanawaza sana mapenzi au ni urahisi wa kujenga hoja. mada za elimu zinahitaji critical thinking na kufanya reference, hivyo wengi hukimbia jukwaa hili
   
 4. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Asante sana kwa kuliona hilo, ila naomba nikukumbushe kuwa hili ndio moja ya mambo yanayonipa wasiwasi mkubwa, Watanzania kudharau yale ya msingi na kushikilia yale yasiyo na tija. Huu ulioufanya ni moja ya mifano na UHAKIKI THABITI wa kile kilicho nifanya niweke post hii hapa. Asante sana kwa kunisaidia kuli-prove hili.
   
 5. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hah ha ha aa!!
  Usinichekeshe ndugu yangu, kukimbia tatizo siyo suluhisho la tatizo husika. Kuna wakati mwingine inatubidi hata kama hatujui lakini ni lazima tu-express kile tusicho kijua ili wengine watujuze. Upo usemi fulani wa kiingereza ambao usemao ".....Whoever knows everything is an Expert in Nothing...."
  Hakuna mtu wala jamii yoyote ile katika historia ya dunia ambayo imefanikiwa katika mambo ya msingi bila kuwa tayari kuumiza kichwa ili kupa jawabu sahii na katika muda sahihi. Kama watanzania hatutaliona hili mapema nina wasiwasi huenda kesho ya watoto wetu ikawa ngumu kuliko leo yetu.
  Hivi tujiulize, kama sio sisi wenyewe....., ni nani basi wakutuletea mabadiliko tunayo yataka???
   
Loading...