Oya wadau kwa anayejua mi ndo nmesikia hvo anihakikishie
bado sana mdau 2lia kwanza labda mwez wa 3 yatakua tayar
Punguza munkari kijana' matokeo yanin sa hiz wakati shule mnatakiwa mwezi July'
Waalimu wanasubiri ajira baada ya kudanganywa na Waziri, wanafunzi wanasubiri matokeo ambayo wanaamini serikali inayoua Elimu itawapa alama.
Punguza munkari, kanuni kuu ni "utavuna ulichopanda".
Oya wadau kwa anayejua mi ndo nmesikia hvo anihakikishie
ongeza sauti tusikie wote!
Matokeo ya kidato cha nne 2013 yatatoka mwezi huu, kwa sababu mwisho wa usajili wa PC ni february 28 kama Necta ilivyotangaza. Lazima yatoke mapema ili wanafunzi wajue kama watarudia mtihani au vipi
TANGAZO
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwakumbusha watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) mwezi Novemba, 2014 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kilichoanza rasmi tarehe 1 Januari, 2014 kwa ada ya Shilingi 50,000/=kwa wanaojisajili CSEE na Shilingi 30,000/= kwa wanaojisajili QT kitaishia tarehe 28 Februari, 2014.
Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa bure na kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au Mpesa.
Imetolewa na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA.
nimesikia TBC leo wanasema wazazi wajiandae...........