Wadai wa CCM wakiwemo wasanii, biashara zao zina leseni halali?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
96,225
168,790
Kwa mfano mtu aliiuzia CCM kofia na t shirts ndo nauliza ana leseni ya biashara hiyo?Au mwingine alikuwa anachekesha na kukatika mauno jukwaani, je anayo leseni?TRA wanamtambua kwa hiyo biashara yake?!Ikumbukwe madai hayo yatalipwa kwa ruzuku ambayo ni kodi zetu so matakwa ya kisheria yahusuyo manunuzi ya Umma ni lazima yazingatiwe.cc H Polepole
 
Na kama hawana leseni basi CCM wanapaswa kuadhibiwa vikali kwa kufanya biashara na wafanyabiashara haramu!!!

Hatuwezi kuwa na taifa lililojaa "wafanyabiashara" na "watoa huduma" wahalifu kwa sababu tu wanafahamu somewhere kuna wanunuzi wahalifu wanaopendaa kununua bidhaa za kiuhalifu!

Tafsiri ya haraka haraka ya mfanyabiashara asiye ni leseni ni kwamba halipi kodi!! Na tafsiri halali kabisa ya mnunuzi anaenunua bidhaa zisizolipiwa kodi ni kwamba nae hataki kulipa kodi... huyu ni mhalifu aliekubuhu kwenye suala zima la ukwepaji kodi!!
 
CCM ndio wafilisi wa hii Nchi......kama unasema ni manunuzi ya UMMA, pia inapasa tujue hiyo tenda ya kunengua na kuchekesha ilitangazwa wapi mpk mshindi akapatikana........ UKIUZA TOA RISITI,UKINUNUA DAI RISTI........huu msemo nadhani CCM hauwahusu.
 
Kwa mfano mtu aliiuzia CCM kofia na t shirts ndo nauliza ana leseni ya biashara hiyo?Au mwingine alikuwa anachekesha na kukatika mauno jukwaani, je anayo leseni?TRA wanamtambua kwa hiyo biashara yake?!Ikumbukwe madai hayo yatalipwa kwa ruzuku ambayo ni kodi zetu so matakwa ya kisheria yahusuyo manunuzi ya Umma ni lazima yazingatiwe.cc H Polepole
Manunuzi ya umma?????? Akili za Lumumba Ni shida....
 
... !Ikumbukwe madai hayo yatalipwa kwa ruzuku ambayo ni kodi zetu so matakwa ya kisheria yahusuyo manunuzi ya Umma ni lazima yazingatiwe.cc H Polepole
Manunuzi ya umma au ya CCM? Je, utaratibu wa zabuni ulizingatiwa? Je, CCM walipata huduma kutoka kwa hao wanaodai kutoa huduma? Acheni dhuluma bana.
 
Kwenye t shirt na kofia CCM hawakuwa na hela wakamkopa mwenye nazo Global Publisher,kunahitajika leseni kwenye msaada?
 
Back
Top Bottom