Wadada wa kazi na watoto wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadada wa kazi na watoto wetu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Somoche, Oct 30, 2012.

 1. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,822
  Likes Received: 921
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu,  Leo asubuhi mida ya saa 12 nimekutana na watoto wadogo 2 wakiwa na mdada wa kazi maarufu kama beki 3 au House girl, nikiwa natoka mazoezini dada yule alikua anawasindikiza wale watoto wadogo kwenda kuanda basi la shule.kwa haraka wale watoto wana umri wa miaka 3 na mwingne 3 na nusu hivi kwa kukisia.kilichonishitua ni kipigo walichokua wanapewa na yule dada asubuhi ile.


  Niliingilia kati kwa kumzuia kwanza asiwapige na baadae nikamhoji kwanini anapiga wale watoto makofi njiani, yeye akasema wanataka pipi, mkubwa akasema sio kweli kanivalisha soksi ina maji na kweli nilipomvua ile soksi nikakuta ina maji, na mimi nikaamua kumzaba vibao na kumgeuza njia kurudi nae japo siwajui nikasimama getini kwao akaenda ndani akaleta soksi kavu nikamvalisha mtoto ndio nikawarudisha kuwahi basi lao la shule.


  Mimi kama mzazi kile kitendo kimenisikitisha sana,kwasababu kuu 2..ya kwanza mda ule wale watoto wadogo wanasaidiwa na kulelewa na Mdada wa kazi tena asiye na uchungu wa kuzaa, matokeo yake anawavalisha soksi zina maji na kipigo. la pili ROHO MBAYA ya watu wa Dar es salaam, watu wa Dar ni watu wana roho mbaya sana japo sio wote maana mda huo watoto wanapigwa kuna watu walikua wanatoka majumbani kwao wakienda kazini na wakawa wanapita tu kama hawaoni, hii ni roho ya mnyama,nawashangaa sana watu wa huu mji ni kama wamechanganyikiwa!!! wito wangu badilikeni nyie wote ni Watanzania..


  NINI KIFANYIKE...Natoa wito kwa wazazi kama mimi jamani hebu wahurumieni hawa watoto wetu, pamoja na kwamba kazi ni mhimu na watu wanawahi vibarua ila kazi ipo na zitaendelea kuwepo je maisha yapo yakishapotea ama kuharibiwa?!! jibu ni kwamba hapana basi kama ndivyo ebu waandaeni watoto wenu, wasaidieni,wahudumieni na mjali afya zao maana nyie ndio wazazi wa hawa watoto, msiwaachie hawa mahouse girl wanatesa sana watoto..


  salaam..
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  hapo wazazi wao wapo busy wanapeana chai ya asubuhi
  hivi mabeki 3 wana akili nzuri 100% hadi uwaamini kuwapa majukumu nyeti ya familia?
  wale ni wasaidizi tu
  ungemwambia awaite wazazi uwalambe makofi sio kumpiga beki 5
   
 3. ram

  ram JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,194
  Likes Received: 898
  Trophy Points: 280
  We mkali, ukamlamba vibao beki 3!

  Ila % kubwa ya mabeki 3 wanaroho mbaya sana, sijui ni kwanini, na pengine unakuta analelewa vizuri tu ndani ya familia lakini kama mzazi haupo watoto wanakiona cha moto
   
 4. snochet

  snochet JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 1,271
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Somoche we jasiri sana,kumzaba makofi stranger si jambo rahisi....sidhani kama kumpiga kumetatua tatizo,ukipata muda,nenda kwa wazazi wa watoto hao jioni uwaeleze,kesho anaweza akarudia,na inawezekana huyo beki 3 akahamishia hasira za kupigwa kibao kwa watoto,wakitoka shuleni.akawaumiza zaidi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye bold hebu tutake radhi kwanza!hivi kwa maisha haya ya sasa kuna mtu anaweza kuingilia famili ya mtu kiasi hicho?kwanza umejipa ujasiri wa ajabu ujue!lakini pia nani anapata uchungu wa kulea mtoto wa mtu ilhali wazazi wake wenyewe wapo wanapeana mahot tube muda huo,kisa dada yupo na atawaandaa watoto!
  watu wapo busy na kulea kazi na nje cup/mume/mke kuliko kulea
  ndo mana siku hizi kesi za watoto kuwa na maUTI ni kama kawaida tu!mtu huna muda na mtoto,huna muda na mahali mtoto anapolala,wala chakula anchokula kisa eti unamlipa mshahara dada!
  af mkirudi huko makazini matusi kibao plus kuwatesa kama wanyama mara mumeo kmashika **** au mdogo wako wa kiume kamnusa kwapa,mara mdogo wako wa kike kampa ka G string afue!hivi mnafikiri hasira zao wanamalizia wapi kama sio kwa hao minors waliopo hapo majumbani!
   
 6. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,822
  Likes Received: 921
  Trophy Points: 280
  Sijawakuta wazazi nimepanga baada ya kutoka huku nakouzia matikiti naenda kwao moja kwa moja jioni ya leo...ni jirani zangu geti la 3 toka kwangu...
   
 7. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,822
  Likes Received: 921
  Trophy Points: 280
  Tofautisha kuingilia familia ya mtu na ubinadamu wa kawaida wa kitoto kidogo cha miaka 3 kupigwa na mtu mzima makofi alfajiri ile, nadhani wewe una matatizo ya akili...au sio mzazi au huna mji unaishi kwa shemeji yako...
   
 8. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  nafikir umenisoma vibaya kiasi hukunielewa!post yangu umeichukulia so personal my dear!nilichokiongea hapo kwa aliye na umakini wa kusoma angenielewa!
  nimeongea kwa uzoefu wa umama nina mabinti wawili(miaka 14 na miaka 7),mke miaka (8)ualimu(miaka 6)udada,uajiri wa hao wasichana,udada wa wategemezi wengine nyumbani kwangu,ushauri wa ndgu jamaa na marafiki
  so yu can save ur abuses my dear!
   
 9. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Mtu anaamka asubuhi saa kumi na nusu au 11 wakati wewe na mumeo mmelala, anawaandaa watoto, na jana alilala saa sita na mshahara ni less than 50,000 ataacha kuwa na roho mbaya. Ni mazingira tunayowapa ndio yanawazidishia hasira na kuwafanya warelay hasira kwa watoto. laiti kina mama wangepunguza ubize kidogo na kujua jukumu la msingi la familia ni lao basi yote haya yasingetokea. Kwa mfano-kuna tatizo gani mama akiandaa nguo za watoto wake usiku akajua kabisa hata nikiwahi kuamka basi watoto watavaa hizi. Au hata kuandaa chai jamani. Maisha ni vipaumbele, kama umeamua kuzaa na kuitwa mzazi basi jua kuna vitu lazima iwe isiwe ni jukumu la mzazi


  Tuliambiwa kwene semina moja kuwa "you can delegate an activity but not responsibility"
   
 10. ram

  ram JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,194
  Likes Received: 898
  Trophy Points: 280
  Kinyau unasema tu, wasichana wa kazi wengine hawabebeki hata aamke saa mbili asubuhi alae saa mbili usiku,kama hayajakukuta unaweza kusema tunawasema vibaya

  Kinyau? MbONA kama wa kwetu wewe?

   
 11. M

  Mundu JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Umefanya vyema...mtoto wa mwenzako ni wakwako.
   
 12. mbota

  mbota JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 741
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  WE JAMAA wewe mkali yani we mkali sana nime penda hiyo bila vitasa hawa mabeki 3 siyo. my suggetion bora wakaka kuliko wadada wandani
   
 13. M

  Msindima JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu hawa wadada hawatabiriki hata umlee kama ndugu yako lazima atakufanyia vituko, unaweza kuamka asubuhi na mapema ukamsaidia kazi zote lakini bado akakunyanyasia mtoto na vituko lukuki mpaka unabaki na maswali yasioluwa na majibu.
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,865
  Likes Received: 6,216
  Trophy Points: 280
  enzi zangu za kulea, uniform za watoto usiku nahakikisha zipo tayari, na mara nyingi nawavalisha mwenyewe..... Sasa sijui wazazi wa siku hizi wanafanyaje.........(ingawa enzi zile hakukuwa na school bus)
   
 15. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  mie mzazi wa siku hizi BD ingawa naondoka nyumbani mtoto bado kalala ila kila kitu chake kinakuwa tayari mpaka maji ya kuoga na ya mswaki,dada ni kumuogesha,kumvalisha na kusubiria school bus tu. kwa hilo na Mungu aendelee kunipa nguvu kwa kweli.
   
 16. Miss-Thang

  Miss-Thang JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Aisee wee umeongea. Fanya hayo hapo juu ndugu.
  Haya malezi yetu ya dot com hayafai kabisa jamani wazazii wenzangu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. HoneyBee

  HoneyBee JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 23, 2012
  Messages: 673
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Watu wengi wamesema inawezekana msichana wa kazi anamalizia hasira kwa watoto na inawezekana ni kweli. Wewe mzee mzima ulijiamulia kumzaba vibao mdada wa watu sababu uliona hataweza kulalamika kwasababu 1) alikuwa anawapiga wale watoto na important zaidi 2) ni msichana wa kazi tu. Niambie, ingekuwa ni mama wa wale watoto ungeingilia umuambie aache kupiga watoto kikatili vile? Ungemzaba vibao na kuja kututambia hapa? Je, kama huyu dada angekuwa si msichana wa kazi bali ndugu anaeishi na familia? I'm not excusing her. What she did was wrong, lakini ungetumia njia nyingine ya kumkanya na kumuambia akambadilishie mtoto nguo. Baadae unaongea na waajiri wake na kuripoti ulichoona. Jukumu ni lao kuamua watakachomfanya. Umewaonesha wale watoto tabia mbaya.

  Pili, ni wajibu wa wazazi kuongea na watoto wao kujua kinachoendelea wakati hawapo nyumbani. Nasisitiza hili jambo tena na tena. Ukweli ni kwamba maisha ni magumu na mishahara miwili ni bora kuliko mmoja, hivyo akina mama siku hizi wanajishughulisha pia na kuwaachia wasichana wa kazi majukumu. Tusilaumu wazazi, bali tushauriane na tuwe macho ya jamii. Ukiona kitu kibaya usisite kuripoti, lakini mambo ya kumpiga mtu mzima acha. Kama ni uchungu na watoto wote tunao lakini hutuoni tunawatafuta wazazi wa watoto wa mitaani kuwapiga makungfuu.


   
 18. andate

  andate JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 2,655
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Huyo ni hafadhali yupo mmoja kwenye miaka kati ya 1983-1986 aligombana na mama mwenye nyumba. Mama mwenye nyumba akaenda kazini kurudi anasikia harufu ya nyama inaungua kwenye oven kufungua anakuta mtoto kabanikwa, housegirl kala kona kitambo.
   
 19. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,865
  Likes Received: 6,216
  Trophy Points: 280
  hongera,
  endelea hivyo hivyo angalau unapata uhakika na nguo za mtoto zipo kwenye hali gani, maana kumwachia hg kila kitu mtoto ataishia kuvaa nguo chafu,   
 20. Catherine

  Catherine JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  omg!! Kuna umuhimu wa kuwa na day care centres sasa, hawa hgs ni majanga matupu.
   
Loading...