Toka nianze kusali makanisa hasa yanayoongoza ibaada kwa lugha iliyokuja na ndege na yale ya mjini kati, kuna kitu kiukweli huwa kinanipa shida sana hasa pale unakuta umekaa na mdada ana min sket inayopita magoti halafu na juu amevaa nguo inayoishia kiunoni tu.
Halafu unakuta hana hata kile kitambaa cha kujifunika hana, shida inaanzia pale anapoanza kuingia rohoni kwenye nyimbo za kuabudu, Mara ananyosha mikono, Mara anainama, Mara anapiga magoti hapo kiuno nje na kama anashanga ndio basi tena akili inasoma mbali ya kijana rijali.
SAA ya mahubiri yuko bize na simu yake ya sumsang na hajali kama amekaa na kijana wa kiume hapo halafu mapaja yako nje balaa, kwa kweli nahisi nitaanza kuwa nawatongoza tu kwani uvumilivu unataka kunishinda.
Au kwenye darasa cha sunday school maana hapo viti vinaangaliana bila hata uoga dada unamwangalia mapaja hata hajali.
NB; WAPO WATAKAOSEMA KANISANI UNAENDA KUABUDU NA SIO KUANGALIA MTU, lakini ukweli ni kwamba macho hayana pazia DADA ZETU TARATIBU KWENYE NYUMBA ZA IBADA. Kwani hata maombi ya kutafuta mke bado sijajibiwa sasa kazi sana.