Wadada ukitoa namba jitahidi kuwa mvumilivu sio kwa Vibomu vya papo kwa papo

Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
2,813
3,767
Habari za wakati huu wanajamvi wenzangu.! Poleni kwa majukumu na Hongereni kwa Kumaliza siku hii kwa amani na kwa wale ambao siku yao haikwenda kama ilivyopangwa basi tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila jambo.
Basi katikapita pita zangu hapa na pale hapa Mjini, nikawa nimekutana na mdada mrembo amenyoa mkato fulani nauelewaga na hata demu yoyote akinyoa huwa najikuta nimenaswa na kuvutiwa mnoo. Dada alikuwa anatembea mie nilikuwa kwenye kaBaby walker kangu nikapunguza speed hadi nikasimama kabisa alfu nikashusha kioo na maongezi yakawa hivi;

Mimi: Mambo mrembo

Yeye : Poaaa

Mimi : Samahani dada unaweza kusogea kidogo hapa kwemye gari

Yeye : Akasogea (She z Kinda of Shy)

Mimi: Samahani dada unaitwa nani vile ?

Yeye : Aziza

Mimi : Oookeiii ...Unaelekea wapi mrembo ?

Yeye : Nipo nipo tu siendi popote

Mimi : Samahani kama hutojali, unaweza kunipa namba yako ?

Yeye : 075.......

Mimi : Ahsante, ngoja nikuflash uipate na namba yangu

Yeye : Samahani naomba miatano

Mimi : (Internally) ila kwa nje nje nili smile nikaangalia hapa pembeni nikaona sina mia tano nikamwambia nina Buku tu. Nikamwambia, anyway haina shida Shika hii hapa

Yeye : Ahsantee

Sasa hapo mimi nikashindwa kumuelewa Aziza, Mbona kuomba namba tu na kuomba Jero . Nimetoka tu hapo nikafuta na namba yake, nimeona kama nimechukua namba kwa Vichuna .

SOMO: Wadada ukitoa namba jitahidi kuwa mvumilivu sio kwa Vibomu vya papo kwa papo daaah
 
Back
Top Bottom