BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,766
- 23,230
Mkuu walikuwa wanafuma kama hobby zaidi, wengi walifuma kwa matumizi yao, fani huwa haifi inabadilika na maisha nadhani, hiyo ni sehemu ya kwanza ya kupeleka; majumbani mwao.
sehemu ya pili:
nahisi hoja yako imelenga kibiashara zaidi. Nasikia vitu handmade huwa ghali zaidi, uliza bei ya picha za kuchorwa pale morogoro stores.
nasikia hata vitu kama viatu au mikanda e.g vya Italy ikiwa handmade ni bei mbaya zaidi.
kuna mdau hapo kasema ni stadi za kazi ambazo hazikurithishwa, nakubaliana naye.
nadhani wangeendelea leo wangeuza bidhaa china kama wao wanavyo tuuzia. virago, wachina nao si wanafuma?
Umeona baba twin eeenh!!!!! simu yng nimeichoka pls ninunulie mpya.
Duh! nimekumbuka mbali, sijui hata kama koroshia bado zinauzwa madukani
Zipo bado.
Unakumbuka tulikuwa tunazinunua kwa namba? Nyembamba,saizi ya kati,nene kidogo,nene sana!!!
siku hizi mambo yamebadilika sana..........
nakumbuka hata zamani hizo mama alikuwa anafuma vitambaa lakin
mara ya mwisho kumuona anafuma tena sijui ni lini
Handmade ni expensive ndio
Ila mitambaa ya kufuma fashion yake imepita
ni nini hasa kilichobadilika?
unataka ya shilingi ngapi?
Hujambo........
Wakuu, kila mmoja apokee heshima kwa stahili yake. wenye mambo! haya, wale wa oyooo poa tu, wa shikamoo pia hali kadhalika.
hebu nipeni maoni yenu kuhusu ulikoishia utamaduni wa kina dada/mama kufuma.
kwenye kumbukumbu zangu bado ipo taswira ya kina mama waliofuma vitu kama soksi, sweta n.k.
Nakumbuka mama yangu alifuma. vitambaa vya meza na makochi nyumbani, hakuwa akinunua alifuma vyake, unakuta akiwa kajipumzisha baada ya kutoka kazini mdogomdogo anahesabu nyuzi hivyohivyo mpaka seti inakamlika.
Na si mama tu, bali hobby ilikuwepo sana zamani kuliko sasa.
Ni nini kilitokea hamfumi tena?
Meza ya ngoma ilikuwa kiboko na unakuta ukutani pamepambwa na Kawa huku imeandikwa penye nia pana njia, Sema life kwa sie wamatumbi inakaba maana kama wazazi wetu wangekuwa na uwezo wa kujenga mjengo wa kueleweka na vi-apartment vya kiana, kulikuwa kuna haja ya furniture za zamani zikawa kwenye moja ya ka-apartment mnakuwa mnatumia kwa kupumzikia huku ukisikiliza muziki toka kwenye player santuri au radio kama memory Q. Lakini ndio hivyo vifaa vyote vya zamani huwa vinapotea potea kutokana na kukosa pa kuviwekamkuu hapo kwenye meza ya ngoma nimecheka sana nazikumbuka.
sweta noma mkuu, fikiria mtu anapanga nyuzi mpaka sweta Linatokea.