angelita
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 3,017
- 2,431
Kuna mambo yanafurahisha hadi huruma.
Nimekaa na mdada hapa anahaha sio kidogo, kapigiwa simu na Bwana wake wakutane hapa sasa kawahi kufika bwana bado ndo kumwambia ale anywe chochote atakacho asihofu anakuja amsubiri atalipa.
Mdada kafanya kama alivyoambiwa tangu saa 6 hadi sasa hivi saa9 jamaa hajatokea na simu haipatikani, anahaha tumbo joto na mfukoni hana hata mia ya akiba, anahangaika kuwaomba ndugu na jamaa wamtumie hela.
Nyie wadada punguzeni kupenda kitonga, kama unaenda sehemu beba akiba lolote likikupata unalitatua, ngoja nione mwisho wake utakuwaje hapa.
Sikukuu Njema wapendwa wangu.