WADADA MI NAPENDAGA TU KUWACHANA LIVE

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,742
Reaction score
25,678
Kama ngono ingekuwa inamfanya mwanaume aowe basi pengine makahaba wote wangekuwa wameolewa maana wengi wako vizuri,inshort hiyo shughuli wanaiweza tena sana tu.

Mwanaume anakaa na mwanamke anayemsaidia sana sio anayefanya naye ngono Sana.
Fikiria namna ya kumsaida mwanaume ambaye Mwenyezi Mungu Amekupa.Dada angu fikiria namna ya kuongeza thamani kwenye maisha ya Mwanaume Mungu aliyekupatia.
Kama ukimuona mwanaume tu kichwani unawaza kudanga,kuchuna,mashindano.Utaishia kujiuliza mbona siolewi ?na kama umeolewa utaishia kusema mbona ndoa yangu haieleweki?
Mungu alimwambia Adam kwamba atampatia msaidizi wa kufanana naye.Sio mtu wa kushinda naye,sio mtu wa kumchuna,sio mtu wa kumchukulia poa poa.... Ukiona upo katika mahusiano na huna cha kutoa zaidi ya ngono,ujue siku zako zinahesabika... kuwa aina ya mwanamke ambaye mwanaume akijitazama ataishia kusema bila huyu mwanamke mimi ningekuwa kenge fulani hivii wa mwituni.
kuna siku raisi Obama aliwahi kulia hadharani machozi ya furaha alipotaja jinsi Michelle alivyokuwa sababu ya yeye kuwa Raisi wa Marekani.
... Chkua point tu my dia...
 
Hahaha na bado ngoma ndo kwanza mbichiiii....

am better here
 
Kwani tunasikiaga basiii, unapoteza tu muda wako kutupigia kelele, sidhani Kama tutakuja badilika, solution Ni wewe kuishi na sisi kiakili Kama huna akili utapata taabu, pole kwa kutendwa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…