Wadada mbona hamueleweki?

Ravalomanana

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2018
Posts
1,677
Reaction score
1,686
Hivi hawa wadada wanaotafuta ndoa kwa upepo wa kisulisuli mbona siwaelewi, ukiwatongoza wanaleta nyodo halafu wanawasumbua viongozi wa dini wawaombee. Sasa lengo lao ni lipi, maana wanaume ndio sisi sisi!
 
wakikataa usiwalazimishe

wakisikia tena mtumishi mwingine ametangaza kimbunga cha kisuli suli

utawaona haooooo..

we waache
 
Wanaume ndio nyie nyie lakini nao wana preferences zao.
Wachungaji hawafanyi maombi ya kuwatafutia mahandsome boy au tall guys,au wenye pesa wanawaombea mpate waume wa kuwaoa sasa umeombewa amekuja humtaki hahaaa
 
Hivi hawa wadada wanaotafuta ndoa kwa upepo wa kisulisuli mbona siwaelewi, ukiwatongoza wanaleta nyodo halafu wanawasumbua viongozi wa dini wawaombee. Sasa lengo lao ni lipi, maana wanaume ndio sisi sisi!
Jamani mi nasiikitika sana, Ratio kati ya wadada na wakaka zinapishana huku wadada wakiwa wengi na wakaka wachache. Mbaya zaidi ni kwamba, tangu hii awamu pendwa wengine wanavyodai, ajira hakuna. Zamani vijana walikuwa wana- plan kusoma masomo ya ualimu wapate kazi baadaye wajiendeleze kwa masomo mengine waukimbie ualimu, siku hizi hata waalimu hawapati ajira. Matokeo yake huku muda haugandi, mida ya kuolewa na kuoa inawadia huku uwezo hakuna.

Hii imekuwa changamoto kwa hapa Tanzania, nchi nyingine sijui. Kwa hali hiyo ndo maana nawahubiri wamejipatia kick ya huu msemo wa kisulisuli. Unakuta namba kubwa ya waolewaji imetimia huku waoaji wako hoi. Lakini kuwa hoi hakumaanishi kila anayesema nakupenda wanakubali on the sport, lazima wajiridhishe na check and balance pia lazima itumike. If you are serious huwezi kutia timu binti akakukataa, labda uwe eidha una ulimi mzito (domo zege), au hujui kuimbisha ( convincing power).
Tena siku hizi unasema kidogo tu, ila ujue utatumia gia gani.
 
Hivi hawa wadada wanaotafuta ndoa kwa upepo wa kisulisuli mbona siwaelewi, ukiwatongoza wanaleta nyodo halafu wanawasumbua viongozi wa dini wawaombee. Sasa lengo lao ni lipi, maana wanaume ndio sisi sisi!
Ukiona unamuelewa mwanamke jua unakaribia kufa.
 
Wachungaji hawafanyi maombi ya kuwatafutia mahandsome boy au tall guys,au wenye pesa wanawaombea mpate waume wa kuwaoa sasa umeombewa amekuja humtaki hahaaa

Ona sasa usivyo na akili...kwani preferences za mtu lazima ziwe handsome na urefu wa mwanaume?

Utapata wa kufanana na wewe,sio lazima kila unapogusa upate
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…