Wadada leo mnisamehe kidogo

Wadada leo mnisamehe kidogo

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,430
WADADA MNISAMEHE KIDOOOGO!

Simwongelei mtu ni ujumbe kutoka kwa mdau wa masuala ya wanawake anaitwa
Lu-Patie!

Wanaume wengi hawajafikia ndoto zao, wanatamani kupata wanawake watakaowatia moyo kuwafikisha kwenye ndoto zao! Ukweli mchungu ni kwamba wanawake hawawataki wanaume ambao bado wako safarini kuelekea ndoto zao! Wanataka waliokwisha fika, na bahati mbaya zaidi waliokwisha fika wako 'occupied !! Linalotokea ni nini?! Wanawake wanadhani wana bahati mbaya ?!

Unaweza kuwa unalalamika kuwa una mkosi WA kuolewa yaani kila mwanaume anakuja na ahadi nzuri, baadae anakuacha! Lakin upande mwingine huenda maamuzi yako ndiyo maumivu yako.

Kweli huenda we ni mtoto WA kike mzuri wa sura umbo na hata kila kitu ila umenyimwa hekima!

Una mpaparikia kijana mtanashati kisa ana gari na kazii nzuri. Unamwona kijana anaeenda kumbi za usiku ndo mjanja..anae vaa suruali chini ya makalio ndo sahihi kwako lakini yule anaeenda ibada kila ijumaa au jumapili unamwona mruga ruga tu!

Una mpuuza Na kumdharau mtu 'A' kisa tu yeye ni kijana aliye soma ila hana ajira. Ama ni kijana ambae kipato chake hakizidi laki 2 kwa mwezi badala yake una mkumbatia mtu 'B' ambae ni baba fulani na ni mume WA Fulani kisa tu anapesa na shida zako zote anakutatulia...!!

SWALI!!
Utaolewa vipi ikiwa mpaka sasa unapenda toka na waume za watu au vijana wenye magari ya mikopo, au kijana yeyote ambaye unajua huna future naye? Au ndo unam'please ili asiache kukupa pesa!? Nani atakae KUOA wakati vijana wanaotafuta mke wewe una wasema vibaya kuwa hawana hadhi ya kutembea na wewe kisa hawana misuli ya uchumi kwa muda huo?

Funguo ya NDOA utaipata wapi wakati hapo ulipo una mnunia mke wa mtu kisa una toka na mume wake?

DADA maisha yanabadilika mwanaume mpiga debe wa Leo kesho unaweza mbadilisha akawa dereva kisha akamiliki gari lake...hakuna MTU aliye zaliwa kuwa masikini ndo maana juhudi zinahitajika...Mwanaume anae tumia pesa kukufanya uwe wake anafanya hivyo kwa wengi ila usijifanye hujui kisa unafaidika jua muda unaenda.

Weka malengo mbele lini unatamani uwe na ndoa na umri gani uzae kuliko anasa. Mwaka WA ngapi huu bado unatoka na wanaume ambao hawana malengo Na wewe, kazi ni pombe na wanawake?

Umegombana Mara ngapi na Huyo HB wako kisa usaliti na bado upo nae?? Wanaume wangapi wenye pesa mvuto na kila kitu ndani lakin wamekutumia na kukuacha? Lakini bado hujifunzi aina ya mwanaume wa kuwa nae?

Japo vyema acha kujidharau u mrembo onesha kwamba unajipenda kuanzia MAVAZI NA KAULI !
Marafiki zako wangapi waliolewa na wanaume WA kawaida lakin Leo wana mafanikio? Kwa nini usiige..weka uzuri pembeni simama imara kama MKE na MAMA bora WA kesho. Mtie moyo mmeo ajisifu kuwa Na wewe, si kila mara dharau Na kumbeza!!

Kifupi hakuna mwanamme anayependa mke asiyemtia moyo kwa kile kidogo anachofanikiwa kufanya !! Encouragement matters most kwa mwanamme yeyote mwenye akili timamu!
 
Wanawake wa aina hiyo, kazi kushinda kwa waganga wawanase wanaume waliofanikiwa, matokeo ni kuwaharibia ndoa na maisha... Karma inawaona
 
You must create your own empire...
sio kudandia dandia waume za watu kama matatu....
kila mwanaume aliefanikiwa ana mwanammke wake... hata kama hajamuoa ,ni mwanammke wake kwa maana ameshiriki kumtengeneza...
hivyo hivyo kwaanaume pia.. waache kudandia wake za watu kama matatu, kila nyuma ya mwanammke anaependeza kuna mwanaume fulani....

ila ni kwa 95% sio wote ,wenginewanajigaramia, wengine wamefanikiwa kama napadre
 
Asante kwa kutukumbusha mkuu! Wanawake tunajisahau saana na anasa za dunia

Tunasahau kuwa muda ukienda haurudi!
 
Duuhh!! Wanasema maneno kuntu huu uzi umetulia najitahidi kuangalia comment naona wadada wengi wanaupita tu huu uzi bila kucomment inaonekana umewagusa sana
 
WADADA MNISAMEHE KIDOOOGO!

Simwongelei mtu ni ujumbe kutoka kwa mdau wa masuala ya wanawake anaitwa
Lu-Patie!

Wanaume wengi hawajafikia ndoto zao, wanatamani kupata wanawake watakaowatia moyo kuwafikisha kwenye ndoto zao! Ukweli mchungu ni kwamba wanawake hawawataki wanaume ambao bado wako safarini kuelekea ndoto zao! Wanataka waliokwisha fika, na bahati mbaya zaidi waliokwisha fika wako 'occupied !! Linalotokea ni nini?! Wanawake wanadhani wana bahati mbaya ?!

Unaweza kuwa unalalamika kuwa una mkosi WA kuolewa yaani kila mwanaume anakuja na ahadi nzuri, baadae anakuacha! Lakin upande mwingine huenda maamuzi yako ndiyo maumivu yako.

Kweli huenda we ni mtoto WA kike mzuri wa sura umbo na hata kila kitu ila umenyimwa hekima!

Una mpaparikia kijana mtanashati kisa ana gari na kazii nzuri. Unamwona kijana anaeenda kumbi za usiku ndo mjanja..anae vaa suruali chini ya makalio ndo sahihi kwako lakini yule anaeenda ibada kila ijumaa au jumapili unamwona mruga ruga tu!

Una mpuuza Na kumdharau mtu 'A' kisa tu yeye ni kijana aliye soma ila hana ajira. Ama ni kijana ambae kipato chake hakizidi laki 2 kwa mwezi badala yake una mkumbatia mtu 'B' ambae ni baba fulani na ni mume WA Fulani kisa tu anapesa na shida zako zote anakutatulia...!!

SWALI!!
Utaolewa vipi ikiwa mpaka sasa unapenda toka na waume za watu au vijana wenye magari ya mikopo, au kijana yeyote ambaye unajua huna future naye? Au ndo unam'please ili asiache kukupa pesa!? Nani atakae KUOA wakati vijana wanaotafuta mke wewe una wasema vibaya kuwa hawana hadhi ya kutembea na wewe kisa hawana misuli ya uchumi kwa muda huo?

Funguo ya NDOA utaipata wapi wakati hapo ulipo una mnunia mke wa mtu kisa una toka na mume wake?

DADA maisha yanabadilika mwanaume mpiga debe wa Leo kesho unaweza mbadilisha akawa dereva kisha akamiliki gari lake...hakuna MTU aliye zaliwa kuwa masikini ndo maana juhudi zinahitajika...Mwanaume anae tumia pesa kukufanya uwe wake anafanya hivyo kwa wengi ila usijifanye hujui kisa unafaidika jua muda unaenda.

Weka malengo mbele lini unatamani uwe na ndoa na umri gani uzae kuliko anasa. Mwaka WA ngapi huu bado unatoka na wanaume ambao hawana malengo Na wewe, kazi ni pombe na wanawake?

Umegombana Mara ngapi na Huyo HB wako kisa usaliti na bado upo nae?? Wanaume wangapi wenye pesa mvuto na kila kitu ndani lakin wamekutumia na kukuacha? Lakini bado hujifunzi aina ya mwanaume wa kuwa nae?

Japo vyema acha kujidharau u mrembo onesha kwamba unajipenda kuanzia MAVAZI NA KAULI !
Marafiki zako wangapi waliolewa na wanaume WA kawaida lakin Leo wana mafanikio? Kwa nini usiige..weka uzuri pembeni simama imara kama MKE na MAMA bora WA kesho. Mtie moyo mmeo ajisifu kuwa Na wewe, si kila mara dharau Na kumbeza!!

Kifupi hakuna mwanamme anayependa mke asiyemtia moyo kwa kile kidogo anachofanikiwa kufanya !! Encouragement matters most kwa mwanamme yeyote mwenye akili timamu!
asantee sana kwa mawaidha adimu
 
Wanawake wengi wa siku hizi wamevurugwa na vyuma kukaza,hata uwaambie nini na maneno gani yenye hekima na busara hawatakuelewa ni sawa mbuzi kumpigia gita,wanachohitaji ni pesa na maisha ya anasa na sio maisha yenye neema ya Mungu,Wanawake wengi wanaamini pepo yao ipo Duniani ndio Maana sio Wavumilivu wa Shida,Wanaangalia leo hawaangalii kesho,wanasema huna pesa leo sikupendi ukipata pesa kesho nakupenda!,nashauri ukiwa kama mwanaume ukikosa mwanamke mwenye mapenzi ya kweli na umri unaona unaenda tafuta Mwanamke yoyote Mzalishe halafu mpige chini kisha uchukue mtoto wako umlee bora stress za kulea mtoto kuliko stress za kulea jitu zima lisilojielewa!
 
Mie nshakusamehe Mjomba. Ila niseme tu ni ngumu sana kumnyoosha mtu ambaye ameshakakamaa.

Pia nikwambie Mjomba maisha ya mahusiano huwa hayajawahi kutafsirika sababu huyo unayemwita "A" mwenye kuhitaji kutiwa moyo inawezekana yote hayo yakafanyika na bado mwisho wa siku ikawa ni sawa na bure yaani anaweza piga hatua na akasahau kabisa alikotoka mwisho wake akawa na tabia kama za huyo "B".

Ndio maana saa nyingine wadada wanajionea kwa nini upoteze muda, hii ndio inasababisha hao watu "B" wawe ni wenye kupendwa japokuwa baadhi yao ni pasua kichwa ila na wazuri pia wapo.

Maoni yangu hao watu "A" wajitahidi tu kupambana sababu ndio dunia tuliyo nayo sasa wanawake wanaotaka kuwa na watu wa kuanza nao chini wapo ila ni wa kuhesabu hivyo wapambane tu kufikia "B" na sio kusubiri eti awe na mwanamke wa kumpa moyo ndio ainuke.

All in all ujumbe umefika.
 
Umesema vizuri sana. Mwenye macho asome na aelewe. Baadhi ya wanawake wanakua na mategemeo makubwa sana kwenye mahusiano lakini wanakata tamaa mapema sana kwa kuangalia kilicho kuwa mbele ya macho yao kwa wakati huo.
 
Nakusaka ww
 
Back
Top Bottom