Wadada jifunzeni kupitia binamu yangu

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,913
Reaction score
67,435
Habari za mchana natumaini wote mmepata runch pale food point au Kilimanjaro hotel (utani tu kama kawaida yangu [emoji1787][emoji1787][emoji1787] Kama bado karibu ugali na mrenda na mtindi huku Bunyokwa)

Twende kwenye mada

Nina binamu yangu ambaye alipata mimba huko mtaani sasa tukakubaliana wanaume wafamilia kumpeleka huyo binamu kwa mshikaji ambaye amempa mimba.

Tulienda na binamu yangu kwa huyo mshikaji tulipo fika tukaongea nae yule mshikaji hakuwa mbishi alimpokea kwa mikono miwili na akatoa faini laki tatu na nusu

Sasa baada ya kumuacha yule binamu kwa mshikaji mimba ikaaza mtia uvivu hataki kupika anamuita jirani yake wanapika pamoja yule jirani sasa yule bwana akanogewa na pishi la jirani huyu binamu wetu huyu ni kweli hajui kupika nikisema hajui kabisa

Sasa mdogo mdogo yule bwana akanogewa kule kwa jirani sasa alipo karibia kujifungua akabidi aje home kuja kujifungua kakaaa sasa siku ya kutaka kurudi kwake ndipo mwanaume akatuma barua kuwa huyo asirudi tena huku hila matumizi ya mtoto nitakuwa natoa

Sasa analia lia kila siku kisa ujinga wake mimi nilimchana nikamwambia hukutakiwa kuruhu mwanamke mwingine ulitakiwa humzoeshe chakula chako ili ajue pungufu lako sasa wewe umempa jirani apike si ujinga huo

Na hii tabia wadada wengi mnayo jifunzeni

Yangu hayo
 
Huyu mwanaume ni mkware tu. Na hii inamaanisha kuwa hawezi kujizuia na wanawake walio karibu naye. Huyu hata akiletwa dada wa kazi hataweza kujizuia.
 
Kaka mwachi umetisha🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 ruch au lunch🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…