Wadada Inawahu... Kila mmoja ajiasses!

Wadada Inawahu... Kila mmoja ajiasses!

sunshine1

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
539
Reaction score
294
Hii mada nimeitoa kwa blog nyingine siyo vibaya kushare na wadada wa JF ili kila mmoja ajitafakari!

.......kwanza nikupongeze kwa kuweka hii siku kuwa ya kubadilishana mawazo na kushauriana,japo mimi ni mwanaume,huwa napenda sana kupitia humu kuchekicheki mambo ambayo kiukweli yamenijenga,na kwa asilimia kubwa najua nini wanawake wanapenda na nini hawapendi toka kwa waume/wenza wao,big up kwako,Leo na mimi nimeona nilete mada yangu hii uiweke........

Mimi ni mwanaume wa miaka kadhaa,,Kilichonipelekea kuleta hii mada ni kwamba kila mwanamke ninayeamua kuwa nae,ananipa majukumu mengi,hata kabla sijamtamkia kwamba nimeamua kuwa nitamuoa,sikatai kwamba kumsaidia mpenzi wako ni jukumu ambalo haliepukiki lakini msaada unaotolewa usiwe ndo kigezo cha uwepo wa mapenzi yetu,kwa kipindi kirefu nimevumilia hili toka kwa wanawake kadhaa lakini sasa naona kama naelekea kushindwa,mimi binafsi najihisi kama nina mkosi vile,kwa heshima yako naomba waeleze wasichana/wanawake kwamba wakati mwingine sisi wanaume tunakuwa na nia kabisa ya kuanzisha uhusiano imara wenye uwezo wa kuzaa ndoa,

ila tunakimbizwa na "mizinga" yao ya kila siku.katika mapenzi kuna kusaidiana,ila naona kama wenzetu wanawake wameona msaada pekee wa kupewa ni pesa,au wao pekee ndo wanastahili msaada,Wanawake wengi huwa wanaharibu uhusiano bila kujua,hakuna asiyekubali kwamba kusaidiana katika mahusiano ni jambo jema linalokubalika,lakini sasa visizidi jamani,si kila siku mtu unakuwa na pesa ya kukupa,na pia ikumbukwe kwamba suala la kusaidiana katika mahusiano si la upande mmoja,sote twawajibika kusaidiana,wanawake wengi baada ya kuwa katika mahusiano huamini kupata mtatuzi wa shida zake zote.mwanaume mwenye nia ya kweli na wewe akianza kukuona unaanza kumgeuza kitega uchumi,taratibu huanza kuzua visingizio vya kutoonana na wewe mwishowe anaishia zake.

Kitu kingine ambacho wanawake hawajui,si kila tatizo unampelekea mpenzi wako,mengine peleka kwa ndugu zako,hivi kila siku mnapotuomba pesa mwafikiri twazitoa wapi?sio wote wauza sembe,wanawake wengine wana kipato zaidi ya wanaume lakini bado hata kile kidogo tukipatacho mwataka,jamani na sie wanaume hatupendwi kuumizwa pasipo sababu,wewe kama ni mpenzi wangu najua wajibu wangu kwamba wahitaji hiki na kile ,sie wanaume hatupendwi kuumizwa pasipo sababu,wewe kila kitu pesa,kwani mimi ndo nazitengeneza?hata kama unahisi ninazo nyingi,basi unadhani zote ni kwa ajili yako?hata mimi nina familia ya wazazi,wadogo zangu nk,nahitaji kuwahudumia,Tuhurumiane jamani,True love means give and take,twawapenda sana wake/wapenzi wetu lakini msitugeuze gari la mshahara,najua tabia hii si kwa wanawake wote,lakini asilimia kubwa ndo hao,naomba kupitia blog hii tujaribu kuwekana sawa,kwa wale ambao wana tabia hizi na mnawajua,waelezeni,mnatuumiza,na ndiyo maana hatuishi kusikia vituko vya kina kaka kuwaachia bili wanawake katika sehemu za starehe,kujifanya wanaenda msalani,kumbe anakimbia kukwepa aibu,kwa maana hela ya kulipa hana
 
Nadhani wakisoma huu uzi wataelewa.mi kuna mmoja nilimwambia ninahitaji kuzungumza nawe baada ya siku tatu kutoka leo,basi siku ya pili akaniambia nimuazime laki 2,sasa nikajiuliza kama nayaka papuch hii ndio bei yake? Nikipata papuch siwezi mdai pesa yangu,je akininyima? Itakua imekula kwangu? Hadi leo tukikutana ananiambia lini utanitafuta,namwambia usikonde mtu wangu.kumbe ndo imetoka hiyo.wanawake they are beautiful by far but,they are far from beautiful.
 
tumekusikia kusikia jomba watalifanyia kazi sababu HAINIHUSU shem wako nsipompa invoice huwa hana hana imani kabisa kwa kujua kuna watu wanamsaidia.
Na hapa kuna invoice anatakiwa ado the needful at the end of this month 1.7m yaani hapa nafikiria invoice ijayo nikujumlishe at least uache lalamika lmao!!!
Tatizo mnavaa viatu size za wajomba zenu matokeo yake vinawapwaya kazi kamshahara kaduchu,matatizo kibao mwanamke unayemtaka mkali balaa nawe unakomaa ili uonekane unamtoto mzuri mjini matokeo yake ndo hayo nadhani ungekuwa na kaundime yasingekukuta haya yaote.
Poleni wanaume jamani mutafute size yenu musife kingereza kufa na tai shingoni.
 
Avoid plagiarism mkuu, hii story iko kwa Sintah blog, acknowledge the source sio kusema 'blog flan' tu, asante
 
Amu,listen dadaa!matumizi yaendane na hali ya maisha,sasa akiwa mtoto mzuri ndo akukomoe? Maisha ndo hayahaya.akipenda high life as a result watu watagonga na kutimua tu,kimyakimya kama mziki wa jay mo.
 
Avoid plagiarism mkuu, hii story iko kwa Sintah blog, acknowledge the source sio kusema 'blog flan' tu, asante

kaka habari weka link twende sawa afu tukutane kijiwe chetu cha ulinzi
 
Sina uhakika sana kama watakuelewa ila kusikia watasikia,tatizo litakuwa kwenye kuelewa maana ugonjwa wa pesa umewakumba wengi
 
Amu,listen dadaa!matumizi yaendane na hali ya maisha,sasa akiwa mtoto mzuri ndo akukomoe? Maisha ndo hayahaya.akipenda high life as a result watu watagonga na kutimua tu,kimyakimya kama mziki wa jay mo.

jamani ujue kuna wanaume wengine kazi wanayoijua kuchomeka tu mtu anakaa lets say kinondoni mdada anakaa mbezi kimara tena makabe anatoka kwao mpaka stand mbezi kubwa na bodaboda 1500 au 2000 stand mbezi daladala za mwenge 500 kutoka pale mpaka huko 400.
Jumlisha hapo hiyo kwenda tu na baada ya hapo mjamaa hata kumtoa nauli tu hakuna khaaa acheni tu mshikwe mkwide tena ukiwakuta waliojichokea anakupiga kabisa hapa Tyta atansaidia kuweka picha.
Jamani mjue hata sie tuna service zetu kwa hiyo mjitahidi kutafuta hela hata kama mwanamke anahela na ana kazi nzuri asikuambie hela ya mwanaume tamu na unajisikia unapendwa na ukajaliwa we mpe tu hata ndogo mpe tena mpe usisubiri akuombe.
Na sie binadamu jamani tunaridhika.
Lakini ukiwa mkavu sana aaaa unaboa hata stimu inakata.
Kama anakuomba sana jiulize ulianzaje nae labda ulianza kwa mashauzi sana au ulimpatia kwa pesa.
Mwanaume mwenye hela ananoga jamani plus umkute kajaaliwa maumbo afu anajua shughuli yake ha ha humkinai jamani ngoja niwaamshe miss chagga Heaven on Earth lara 1 akitoka jela atakuja miss strong waje wansaidie labda mtaelewa darsa cc Paloma
 
Last edited by a moderator:
Ukijipeleka kihela hela basi uwe tayari kuzitoa. Tofauti kati ya mapenzi ya hela na ya kweli ni kuwa; mtu umekutana na mwanamke leo, unataka muwe wapenzi kesho, na mkagegedane kesho kutwa. Hakuna mapenzi hapo ni hela tu.
Kama kweli unataka kuanzisha mahusiano ya kudumu na mtu na hutaki yahusishe hela basi yape mda. Mda wa kujuana, kuzoeana, kusomana nk.
Matumizi ya hela nayo yana mawili; unaweza kutumia hela ukaishia kugegedana baasi, lakini pia hela zinaharakisha kujuana kusomana nk kwani zinawaweka karibu kwa haraka zaidi...

Kwa hiyo kama una hela unaweza kuzitumia wisely kuanzisha mahusiano ya kudumu lakini hata kama hauna, zipo njia mbadala japo zahitaji mda...
 
jamani ujue kuna wanaume wengine kazi wanayoijua kuchomeka tu mtu anakaa lets say kinondoni mdada anakaa mbezi kimara tena makabe anatoka kwao mpaka stand mbezi kubwa na bodaboda 1500 au 2000 stand mbezi daladala za mwenge 500 kutoka pale mpaka huko 400.
Jumlisha hapo hiyo kwenda tu na baada ya hapo mjamaa hata kumtoa nauli tu hakuna khaaa acheni tu mshikwe mkwide tena ukiwakuta waliojichokea anakupiga kabisa hapa Tyta atansaidia kuweka picha.
Jamani mjue hata sie tuna service zetu kwa hiyo mjitahidi kutafuta hela hata kama mwanamke anahela na ana kazi nzuri asikuambie hela ya mwanaume tamu na unajisikia unapendwa na ukajaliwa we mpe tu hata ndogo mpe tena mpe usisubiri akuombe.
Na sie binadamu jamani tunaridhika.
Lakini ukiwa mkavu sana aaaa unaboa hata stimu inakata.
Kama anakuomba sana jiulize ulianzaje nae labda ulianza kwa mashauzi sana au ulimpatia kwa pesa.
Mwanaume mwenye hela ananoga jamani plus umkute kajaaliwa maumbo afu anajua shughuli yake ha ha humkinai jamani ngoja niwaamshe miss chagga Heaven on Earth lara 1 akitoka jela atakuja miss strong waje wansaidie labda mtaelewa darsa cc Paloma

Mtu huwezi kujizuia kabisa kutumia hela kwenye harakati za mapenzi. Tatizo linakuja pale mtu anapokuwa anawapima wanaume kwa kiasi cha hela wanachotoa, na sio thamani ya mapenzi wanayoonyesha...
 
Last edited by a moderator:
Mtu huwezi kujizuia kabisa kutumia hela kwenye harakati za mapenzi. Tatizo linakuja pale mtu anapokuwa anawapima wanaume kwa kiasi cha hela wanachotoa, na sio thamani ya mapenzi wanayoonyesha...

hapo kweli kuna biashara mkubwa.
 
^^
Wanawake wanaojua mapenzi yasiyoambatana na pesa,, WALIKUWEPO.
^^
 
tumekusikia kusikia jomba watalifanyia kazi sababu HAINIHUSU shem wako nsipompa invoice huwa hana hana imani kabisa kwa kujua kuna watu wanamsaidia.
Na hapa kuna invoice anatakiwa ado the needful at the end of this month 1.7m yaani hapa nafikiria invoice ijayo nikujumlishe at least uache lalamika lmao!!!
Tatizo mnavaa viatu size za wajomba zenu matokeo yake vinawapwaya kazi kamshahara kaduchu,matatizo kibao mwanamke unayemtaka mkali balaa nawe unakomaa ili uonekane unamtoto mzuri mjini matokeo yake ndo hayo nadhani ungekuwa na kaundime yasingekukuta haya yaote.
Poleni wanaume jamani mutafute size yenu musife kingereza kufa na tai shingoni.
Hizo za mapedeshee zinakuaga tamu, ila mwisho wake sasa ndo mtafutano.
 
Installing Love .
████████░░░░░░░░░░░░ 39.5%.....Installation failed.
Error http 404: Install Money first.
Hahaaaa hawezi kubadilika. Yaani wao wakishapata bf ndo baasi matatizo yote kwake.
 
Huyo mwanaume mchoyo

Au anawanawake ambao sio kiwango chake
 
Back
Top Bottom