Wadada beware of destiny

Wadada beware of destiny

Samcezar

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
13,096
Reaction score
22,826
Naandika hii post kwa hisia nzito kwa watoto wa kike especially ambao wameshapevuka na wamevuka umri wa miaka 18.

Okay ni hivi destiny kwa kiswahili ni hatima au mwishoni.

Akina dada nawapenda sana hadi kuwaambia maneno haya mazito, dada zangu mdada unapokuwa unafwatwa na wanaume wengi haimaanishi wote ni wako bali unatamaniwa.

Kuna mdada hapa mtaanaani alikuwa ni mkali balaa siku za nyuma ila sasa stress za upweke zinamharibu muonekano anakuwa kama mzee na hata akili yake now sidhani kama ipo sawa ingawa ana elimu kiwango cha degree.

Huyu dada alikuwa strict mbaya sisemi alikuwa anaringa. Miaka ya nyuma kila aliyekuwa anamtaka alichezea cha mbavu. Alikomaa na shule tu akirejea likizo ni ndani muda wote.

Sidhani kama huyu dada alikuwa na mtu, miaka ikapita watu tukawa hatumuone tena kitaa wajanja tukajua tu kuwa goma limebebwa mazima na jinsi alivyokuwa mkali.

Sasa juzi kati nimetimba kitaa kijiweni namuona anapita kamshika mtoto wa kama miaka 9 hivi. Wadau wakanitonya kuwa wanamuona mbona longtime alirudisha majeshi home kwao kwa bi mkubwa life la ndoa limezingua.

Akarudi kitaa akazuga miezi michache ghafla akaanza kurudishwa na audi ya mume wa mtu.........mwenye mume aliwafumania huko akagawa dozi kwa bi dada ongezea na mikasa miwili mitatu ya kutoka na njemba tofauti zilizompotezea muda kisha zikamwacha solemba.

Sasa bi dada yupo kitaa tu hayupo sawa si tena yule ninayemjua uzuri unafifia mwanzo alikuwa mkimya na haonekani kitaa ila now anaongea huyo kama chiriku.

Yupo yupo tuh busy for nothing church kwa sana.Nikashika tama nikasema mmmmmmmmmmhmn kweli binadamu tunapanga ila yupo anayeamua hiyo mipango iwe ama isiwe.

Usifanye mchezo na destiny
 
Cha ajabu ni nini? Kumbe aliolewa, ana mtoto, na wameachana na mumewe karudi kwao. Sasa hapo ni ajabu? Kama aliona maisha ya ndoa yanamzingua, ulitaka afanyaje?
 
umbea mwingine jamani khaaa! kweli ni kipaji
 
Hii mada hainihusu, nimepita tu.

Ila ki ukweli watu type ya huyu ndugu mwandishi ndio wanaonifanya nisitake mazoea mazoea kabsa na watu nliokulia nao kitaa kimoja i.e. wakubwa kwa wadogo wote.

Yan ni umbea umbea na kufatilia ya watu tu. Kuna watu unakuta huna mazoea au story nao yet wanajua issue zako zooote, nnje ndani. Huwa nashindwaga kuelewa inakuaje mwanamme unakua na mikato hiyo. #Rubbish .
 
Mleta mada ni balaa! Ila kuna kaukweli flani hivi aisee.
 
I figure you having girls' issues, i feel bad for you son/
You got 99 problems, and b!tching's the main one/.....hit me!


Where's Rick?? I'm in the zone baby. Need a beat.
 
Nilifikiri una ujumbe mzito na usia wa kueleweka kuhusu dhana nzima ya destiny kumbe u Shigongo tu. Aaaaargh!!!
 
Yaani sijategemea mwanaume mzima unaumiza vidole na kupoteza bundle yako , kwa ajili ya ku type umbea , tena unaomuhusu mwanamke wa mtaani , yaani katika zama hizi kumbe viumbe hivi bado vipo , wewe mkaka hembu badilika acha tabia hiyo si njema na pia ni viashiria vya tabia nyingine mbaya zaidi.
 
We ushaoa lakini? Make bado upo kitaani kwenu hadi leo, au bado upo upo kwa mama wala ugali wa shkamoo?
 
We ushaoa lakini? Make bado upo kitaani kwenu hadi leo, au bado upo upo kwa mama wala ugali wa shkamoo?


Ninakaa kwangu jembe........kitaa changu huwa nakwenda wapa hi wana pia tuna kijiwe chetu cha longtime sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom