Wachumi wetu Hazina na BOT wanafanya nini kuiokoa shilingi yetu au mpaka Magufuli awape TOR ndipo “waamke” usingizini? II

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,466
2,860
Wakati wa kufungua mji mpya wa serikali ya JMT na nyumba za “wanene” wa nchi hii, Rais wa JMT akawa na furaha kwa kazi nzuri ya Col. Charles Mbuge. Kwa kuwa Rais ndiye CiC,hapo kwa hapo akatoa maagizo ya kupandishwa cheo Col. Mbuge na kuwa Brig. General, kwa Marekani angekuwa anaitwa “One Star General”

Hilo liliwezekana ndani ya siku hiyohiyo wala halikuchukua muda na hapakuwa na longolongo.

Wakati anazindua Hospitali ya Rifaa na Chuo huko Mloganzila, Rais akaponda sana kwanini NHIF wanaingeza mapesa kwenye miradi ya majenzi. Palepale akatoa maelekezo kwa Watanzania wenye vision na Outstanding business plan za viwanda vya vifaa tiba, wamtafute Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ili kupata mikopo au dhamana ya taasisi hiyo. Kwa kuwa wanaofanya kazi hapo ni raia, na sio wapiganaji, bila shaka kuna kupigana “sound” in the name of ”michakato”…hawa ndiyo Watanzania. Kuzungushana kwa kile inaitwa umangi meza hiyo nayo yaweza kuwa conspiracy mambo yasiende wakati wapo Watanzania toka Namba moja kasema, kungekuwa na kiwanda kishasimikwa na kinazalisha.

Najaribu kukumbuka tena wakati mmoja JPM alisimulia namna alivyomfuata Rais Mkapa na kumwomba amkubalie aipeleke kwenye cabinet nmoja kwa moja hoja ya kukusanya fedha za ndani ili kujenga barabara kupunguza kutegemea mikopo na misaada ya “wajomba wa ughaibuni”. Kwa maelezo yake walikubaliana na Rais Mkapa, mchakato ukianzia Wizarani kwa wataalamu then kwa makatibu wakuu, ingepigwa chini kwa sababu "nzuri kabisa za kitaalamu". Rais Mkapa akamkubalia aiweke vyema hoja yake, ilipokwenda kwenye cabinet, mawaziri wengi wakaipiga chini. "Mkuu wa kaya" wa wakati huo akaunga mkono hoja ya JPM licha ya kupingwa na majority ya cabinet; hivyo ndivyo TANROAD akiwa moja ya wakala yenye “mpunga” wa kutosha kujenga barabara za Tanzania. Tafsiri rahisi aliyotupa JPM ni kuwa “wachawi” walikuwa wataalamu na mawaziri wenzake. Tanzania huwa kuwa vitu vizuri vinapigwa chini na kukwamishwa in the name of policies, procedures, michakato, kanununi....

Tunaweza kujiuliza, kwanini jambo likiwa mikononi wa wachache na wakalisimamia linakuwa na positive effect hasa kama wale wachache walipangilia kwa umakini. Ngoja tuendelee kudadavua mambo.

Stephen Covey mwandishi wa kitabu cha 7 Habits of Highly effective people anasema "I am not a product of my circumstances. I am a product of my decisions." Nikichukua alichokisema katika Muktadha wa ajira Tanzania, ajira sio matokeo ya circumstance, ni zao la maamuzi ya kutojali ya kizazi kilichopita cha decision makers ambao walitakiwa kujenga daraja ili kizazi cha sasa kisi-undergo dead end baada ya masomo ya vyuo vikuu na vyuo vya kai. Kwenye sanaa ya kuamua, hata kutokuamua nako ni kuamua.

Inapofikia vijana wanataka fursa ya kutumia akili yao na nishati yako kuzalisha. Kazi kubwa ya viongozi ni kujenga platform ili wahusika waingie “kizigoni” wazalishe. Kwa yeyote yule mwenye basic knowledge ya Human Resources, muajiri humlipa mfanyakazi mshahara wake ukiwa sehemu ya gharama za uendeshaji wa kampuni/taasisi.

Napata tabu sana ninapoona wanakuja wanadamu waliozaliwa na wanawake toka ughaibuni, halafu baadhi ya viongozi wetu wanawapeleka kwenye bohari za pamba, kahawa, korosho, mahindi na tunajivunia kuuza malighafi. Hao ngozi nyeupe wanapochukua, wanakwenda kuweka kwenye viwanda ambavyo sisi kama nchi tunaweza kuvinunua, na in-turn wakulima wetu wanakuwa sawa na vibarua wa kuzalisha mazao ghafi ya viwanda na kutoa ajira kwa wenzetu huko ughaibuni. Sie tunabakiwa kuwapiga “sound” vijana ohh, sio lazima uajiriwe. Hao wanaosema hivyo, wengi wao, hawajawahi hata kukaa mtaani na kujua ugumu wa kitaa jinsi ambavyo sio rahisi kutengeneza ajira endelevu kwa kubaingaiza. Sio rahisi kama hao wanaosema wanavyofikiri.
Duniani kote huwezi kujenga jamii endelevu yenye kujenga mifumo ya kitasisi kama mifuko ya bima na mifuko ya pensheni kwa kutegemea "ma-day waka" wanaofanya uchuuzi mtaani au wamiliko wa viduka na viosk.

Mwaka 2017 wakati wa kusoma bajeti ya Uvuvi na Mifugo, waziri alitamka kuwa sekta ya uvuvi imeajiri zaida ya watu milioni 4. Kama moja ya tatu ingekuwa kwenye mfumo rasmi wa ajira na kuchangia kwenye mifuko ya pesheni, fedha zao kupita kwenye mifuko ya kibenki wapete mikopo kujenga makazi bora hali kadhali kuwaingiza kwenye mifumo ya bima ya afya. Bahati mbaya mufumo ya uvuvi inatumia teknolojia dhaifu na kwa asilimia kubwa wengi ni wazalishaji wa kupata hela ya kula, then kesho pia wahangaike. Huu mfumo sio sawa kwenye karne ya 21.

Kwa akili ya kawaida, kwa kuwa nimeonesha kuja jambo haliko sawa hasa kwa watu wanao-set policies, ni vyema kuja na suluhisho hapahapa ili tupunguze vijana wetu kitaa na kutumia akili yao kuwa busy kuzalisha kwa tija na uzalishaji endelevu. Natoa mtazamo wangu kama layman. Nategmea muunganiko wa kisomi wenye kutoa majibu toka kwa decision makers na sio "kupigana sound"

Mathalani, Waziri Luhaga Mpina alisema Tanzania ina upungufu wa maziwa na kila mwaka tuna-spend zaidi ya billion 30-50. Hizo fedha zinaweza kubaki hapa kwa Wizara kuita wenye “akili” ya namna gani ya kuja na mpango mkakati wa muda mfupi na muda wa kati ili hizo fedha zibaki humu ndani. Tunajua hata huko mko wenye akili sana tu, ila wito huu ni kuomba ku-join forces ili kuijenga Tanzania ambayo ni yetu sote.

Tukikubakiana kufanya kazi kwa pamoja, athari yake ni kuzalisha maziwa kwa wingi ndani ya Tanzania. Ajira zitapatikana, tax base ya TRA itaongezeka, vertinary inputs zitanunuliwa za ndani, madaktari wa mifugo wa ndani watakuwa na ajira au wanakuwa ma-consultant kwenya mashamba ya mifugo. Magari ya kusafirisha maziwa yatatoa ajira kwa Watanzania. TFDA, TBS, TANESCO, Idara ya maji wote hawa ni directly stakeholders wa uwekezaji huu. Mifuko ya bima ya afya, mifuko ya pensheni, wote hawa ni stakeholders.


Leo, akitokea Lushinge akaenda na andiko la kibiashara na anajua how to make such a milk processing industry happen, Je, wakubwa wetu wanaweza kumsikiza, na kama watamwelewa, je wako tayari kusimama nae to make the investment happen? Najaribu kuwaza, kama JPM na Rais Mkapa wakati huo walijua “proposal” ingeanzia kwenye level ya wakurugenzi, then makatibu wakuu, then cabinet ingeweza kukwama, inakuwa vip kwa Lushinge? Akina Larry Page wa Google, akina Mark Zuckeberg wa facebook walikuwa na project ambazo hazikuwahi ku-exist. Kwenye agro-processing Tanzania twahitaji dhamana ya serikali ili tukimbie kwa haraka kufikia uchumi wa kati 2025.

Ninamjua mtu mmoja ana mradi wa uwekezaji unataka kufanana kiasi na huo hapo juu ila mpaka sasa, imekuwa kazi kubwa kweli kuwapata akina Luhaga Mpina japo wakae mezani.

Okay, tuje na assumption ya pili. Pitia tovuti hizi hapa then naomba tufikiri pamoja

8 Of The Most Expensive Fruits In Japan
People in Japan are paying thousands for pieces of fruit

Vip kama tukikaa na Japan na kuomba japo tupeleke sweet melon million 10 na black waater melon mil 10 kila wiki. Na tuwe na simple assumption ya kuuza kwa sh. Elfu 15 kwa kila tunda. Hizi ziwe ni hela zinamrudia mkulima mkononi, zingine zinaingia kwenye logistics, insurance, wao wajapani waendelee kuuziana kwa hizo dola kati ya USD 25 na kuendelea. If we could make that happen, Tanzania ingekuwa inaingiza kwenye mzunguko Trilioni 7.8. Tuje na assumption, kwa kuwa Serikali kupitia wizara ya fedha, kilimo na uchukuzi itaweka dhamana yake ili wakulima wakopeshwe fedha in term of irrigation technology, training, agro-inputs, na mengineyo… ili yenyewe ikate 30% ya fedha yote, kwa uchache TRA atakuwa na chanzo kipya cha TRIL 2.6. Ukiunganisha na indirect taxes as a result of deductions za kweny umeme, maji mafuta (watajaza wenyewe).

Ukija na mradi kama huu, watu serikalini wengi wao, (sio wote) watasema, haya mambo sie hatuwezi. Ila Waziri Mpango anaweza kukopa toka Japan huko huko tujengewe barabara na miradi ambayo athari yake ya kukuza na kusisimua mzunguko wa fedha kukuza uchumi, inachukua muda mrefu…. Kwangu mimi, mradi wa kimkakati ningewatafuta wadachi na Waisraeli ambao wanafanya mambo kama hayo, nikae nae ili wa-make that kind of investment happen in Tanzania settings.

Naunga mkono ujunzi wa barabara, viwanja vya ndege, kununua ndege ujenzi wa reli na ujenzi wa Stiglaz… Ila nashauri, kama kuna uwezekano, tukae na namba moja ili na mambo yanayoweza kusisimua na kuleta fedha kwa haraka yafanyike. Nguvu ya ufalme ni jeshi lake lenye nguvu. Nguvu ya uchumi wa mfalme ni kujenga wapiganaji wenye uwezo wa kununua bidhaa na huduma baada ya kuzalisha. Fursa za kuzalisha bado zipo, haitawezekana kwa technology ya mwaka ’47…

Namba Moja, huko uliko, fikiria namna ambavyo ulitumia unconventional methodologies kufanikisha project zako wizarani, nasi huku, tuna namna ya kukupa michongo mbadala ya kimkakati ku-speed up collection ya revenue kwenye chungu chako. Mkakati wa Prof. Luoga (Gavana BoT) kuzua na kufunga maduka ya ubadilishaji fedha ulikuwa mzuri, ila kuna haja ya kuja na miradi ya uwekezaji ya kuongeza exports kwenye sekta ambazo tuna competitive advantage. Mkakati wa kuuza agro-finished products sokoni na sio agro-raw material

Namba moja, kuna conspiracy za kukwamishana kibongobongo ambazo nawe ulizi-experience ukiwa Waziri. Iko haja kupata strategic investment project zenye quick rate on return ambazo zinaweza kabisa kufanyika Tanzania; ili wakati huo wewe unapiga hiyo “ma-miradi” ya kujenga reli, stiglaz, mabarabara, maviwanja ya bombardier na mengine mengi.

Shalom
 
Wenzako hawana akili hiyo zaidi ya kuwaza kuuenzi mwenge na kuhakikisha wanabaki madarakani. Hayo mainvestmeny ni ya wazungu.
 
Sidhani kama mtu mwenye kadi ya CCM anaweza kuwaza hivi ulivyowaza...
 
Wafanye nin na wao ni wachumia tumbo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, Bado naamini kuna kuna wazalendo wapo ambao mambo haya yakifanikiwa, kuna namna wao pia watafidika.
Na kama kuna wachumia tumbo, tuwaombe wa-facilitate michakato ili investment zikianza kutema, definately kodi itaongezeka; na kwa kuwa imeongezeka watazidi kufaidi zaidi.

Standard Bank ya South Africa baada ya kuwa reserve ya mauzo ya dhahabu na Almasi ya Kusini mwa jangwa la Africa, iliweka mazingira rafiki ili communit ya wazungu wafaidike na zile hela kwa kuzifanya kiwe accessible wakope na wawekeze ili kukuza uchumi.
Kuna namna ikifanyika, wakubwa huwa wanafaidi zaidi
 
Sidhani kama mtu mwenye kadi ya CCM anaweza kuwaza hivi ulivyowaza...
Mkuu
Maendeleo hayana chama, na umasikini ni mbaya, athari yake sio rafiki kwa maslahi mapana ya Tanzania yetu.
Enzi ya mwl. CCM hao hao kama chama na taasisi zake za UVCCM, Wazazi na UWT waliwekeza kwenye property development kwenye maeneo ya kimkakati. Leo hii kuna majengo wanapangisha kwa yeyote yule.

Hata wao kama wana utayari kwa kutumia dhamana ya assets walizo nazo tunawashauri wawekeze kwenye miradi kama hii, eventually kuna namna huo mzunguko utamgusa Mtanzania yeyote. Tukianzia hapo huo ndiyo mwanzo wa UZALENDO wa kweli
 
Mkuu, Bado naamini kuna kuna wazalendo wapo ambao mambo haya yakifanikiwa, kuna namna wao pia watafidika.
Na kama kuna wachumia tumbo, tuwaombe wa-facilitate michakato ili investment zikianza kutema, definately kodi itaongezeka; na kwa kuwa imeongezeka watazidi kufaidi zaidi.

Standard Bank ya South Africa baada ya kuwa reserve ya mauzo ya dhahabu na Almasi ya Kusini mwa jangwa la Africa, iliweka mazingira rafiki ili communit ya wazungu wafaidike na zile hela kwa kuzifanya kiwe accessible wakope na wawekeze ili kukuza uchumi.
Kuna namna ikifanyika, wakubwa huwa wanafaidi zaidi
Wanajua hayo ila wameridhika na njia wanayopitia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom