real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,292
Wachumi nchini wamesema ni hatari kwa Serikali kufanya uamuzi bila kushirikisha wafanyabiashara au vyama vyao kwa kuwa wanaweza kuwa kiini cha nchi kuyumba kiuchumi.
Baadhi ya wasomi hao, wakijenga hoja zao kwa kuonyesha wazi tofauti za kimtazamo wa biashara na uchumi wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne iliyokuwa chini ya Jakaya Kikwete, na ya awamu hii ya Dk John Magufuli, wamesema maamuzi yanayowashirikisha wadau yana afya zaidi na ni mtaji mzuri kwa Serikali kuweza kujipanga. Walishauri Serikali itumie mbinu za ushirikishwaji badala ya mbinu ya mapambano.
Wachumi hao wametoa maoni yao wakati Serikali ikipambana na wafanyabiashara kwa kuwatuhumu kuwa wanaficha sukari pamoja na ukwepaji kodi.
“Kimsingi inapaswa kuwepo mbinu shirikishi. Serikali inapochukua uamuzi bila kuwahusisha wadau inakuwa imekwenda kinyume na misingi ya biashara,” alisema Profesa Prosper Ngowi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe. Alisema Serikali inaweza kuwa haijui baadhi ya mambo ya uchumi na biashara, hivyo uamuzi wowote usiowahusisha wadau unaweza kuikosesha Serikali elimu ya kuyajua mambo hayo yanayoweza kuwa msaada kwa uchumi wa nchi.
“Mfano ni suala hili la sukari; wadau wangeweza kutoa ushauri wa bei ya bidhaa hiyo, na hii si kwa sukari pekee bali kwa masuala yote muhimu ambayo wadau wapo na wanapaswa kushirikishwa,” alisema na kuongeza kuwa wadau hao wa sukari wangeweza kushauri jinsi soko la ndani la sukari lilivyo kabla ya kuzuia uingizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje.
Chanzo: Mwananchi