St. Paka Mweusi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 7,639
- 4,526
Kazi unayo atakayewahi kujibu hiyo signature yako.
Msaada tutani wakuu,wakati kiwinta kimekolea huko nje na hata kutoka siwezi nimekaa hapa sitting room kwangu nafikiria kisa kilichonikumba.Kisa hicho hakina tofauti na kile kilichoimbwa na marehemu Mbaraka Mwishehe.
Nimepata wachumba watatu,nataka kuoa mmojawapo,na wote ni wazungu.Kila mmoja ni mzuri sana ila tabia zao ndio shida,wa kwanza ni mvivu hata kutoa sahani yake aliyolia chakula kupeleka jikoni inamshinda,wa pili ni mbea kila siku kuzusha maneno,na wa tatu ni mlupo wa ajabu kiasi kwamba kaniambia yeye ni sex addict na akikosa hata siku moja tu anaweza kupata hysteria.Sasa jamani nisaidieni mimi,nimuoe yupi?
Mke mwema/mume mwema hutoka kwa Mungu Paka Mweusi,
Muombe Mungu kwa bidii na kwa kumaanisha.
Ikiwa ktk hao watatu mke wako yupo, atakuambia, Na ikiwa hayupo atakwambia pia.
Halafu atakupa yule ambaye ni mke wako, ambaye ukimwona utasemaaaaa,
Hakika huyu ni nyama katika nyama zangu na mfupa katika mifupa yangu.
Kama huwezi kuwabadilisha wawe kama unavyotaka, basi tafuta wa NNE.
rudi uone nyumbani
Mungu alisema tuwe na wachumba wangapi ili tuchague mmoja kati ya hao?
ila na wewe ni kiwembe.....watatu kwa wakati mmoja na wote unawagawia uroda.......duh....mi naona uchukue huyo mlupo kwa sababu mna katabia kanaendana.....atacover nafasi za hao wengine
chagua kwa kuangalia positive elements za kila mmoja. Approach yako ya kuangalia makasoro ni approach ambayo haitakupa jibu sahihi kwani hakuna mwanadamu asiye na kasoro. Ila pamoja na kasoro zao tunavutwa na mengi sana waliyojaliwa na Mungu, na hasa upendo, uvumilivu, usikivu, upole, nk. kwa kutaja machache.
Mungu hajawahi kusema tuwe na wachumba wangapi AMA, ila Mungu anatoa mke au mume, uchumba ni hatua ya kufikia kwenye ndoa.
Lakini kwa case ya Paka mweusi tayari ameshanasa kwene mtego wa kuwa na mabinti watatu, lkn kila mmoja anaona kasora kwake.
Kwa maana ingine akili yake imefika mwisho ktk kuamua yupi mke.
Sasa kwa sababu ndoa ni taasisi nyeti sana, hana budi kumwomba Mungu msamaha kwa kukosea kuwaweka wadada kwenye quee, then amuombe ampe mke mwema.
Kama yupo katika hao na iwe, kama hayupo, na apewe mke wake.
Au paka Mweusi we unasema je baba???
Babuyao kasoro hizo za hawa wachumba wewe unazionaje?
Basi mwambie paka mweusi aache kuchakachua wasichana kisaikologia kama sio kimwili kwa kigezo cha kutafuta mchumba.
Kama Mungu amempa kila mmoja wetu mwenza, na tutulie, tusubiri ufunuo.