Wachumba watatu.

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,401
2,000
Msaada tutani wakuu,wakati kiwinta kimekolea huko nje na hata kutoka siwezi nimekaa hapa sitting room kwangu nafikiria kisa kilichonikumba.Kisa hicho hakina tofauti na kile kilichoimbwa na marehemu Mbaraka Mwishehe.
Nimepata wachumba watatu,nataka kuoa mmojawapo,na wote ni wazungu.Kila mmoja ni mzuri sana ila tabia zao ndio shida,wa kwanza ni mvivu hata kutoa sahani yake aliyolia chakula kupeleka jikoni inamshinda,wa pili ni mbea kila siku kuzusha maneno,na wa tatu ni mlupo wa ajabu kiasi kwamba kaniambia yeye ni sex addict na akikosa hata siku moja tu anaweza kupata hysteria.Sasa jamani nisaidieni mimi,nimuoe yupi?
 
LD

JF-Expert Member
Aug 19, 2010
3,015

Mke mwema/mume mwema hutoka kwa Mungu Paka Mweusi,
Muombe Mungu kwa bidii na kwa kumaanisha.

Ikiwa ktk hao watatu mke wako yupo, atakuambia, Na ikiwa hayupo atakwambia pia.
Halafu atakupa yule ambaye ni mke wako, ambaye ukimwona utasemaaaaa,

Hakika huyu ni nyama katika nyama zangu na mfupa katika mifupa yangu.
 
Nanren

JF-Expert Member
May 11, 2009
1,919
2,000
Kama huwezi kuwabadilisha wawe kama unavyotaka, basi tafuta wa NNE.
 
Mapinduzi

JF-Expert Member
Aug 23, 2008
2,424
0
Mke mwema/mume mwema hutoka kwa Mungu Paka Mweusi,
Muombe Mungu kwa bidii na kwa kumaanisha.

Ikiwa ktk hao watatu mke wako yupo, atakuambia, Na ikiwa hayupo atakwambia pia.
Halafu atakupa yule ambaye ni mke wako, ambaye ukimwona utasemaaaaa,

Hakika huyu ni nyama katika nyama zangu na mfupa katika mifupa yangu.

Mungu alisema tuwe na wachumba wangapi ili tuchague mmoja kati ya hao?
 
Matarese

JF-Expert Member
Aug 30, 2009
528
225
Rahisi mkubwa, kwanza weka vigezo vyako wewe unamtaka mwenye vigezo vipi. Then chora table au tengezeza bipartite graph kuonyesha yupi anafit vigezo vipi. Yule atakayetoa maximum perfect matching kwenye table au graph yako chukue yeye. Kama hujui jinsi ya kutengeza bipartite graph niPm nitakuonyesha. Cheers.
 
LD

JF-Expert Member
Aug 19, 2010
3,015
2,000
Mungu alisema tuwe na wachumba wangapi ili tuchague mmoja kati ya hao?

Mungu hajawahi kusema tuwe na wachumba wangapi AMA, ila Mungu anatoa mke au mume, uchumba ni hatua ya kufikia kwenye ndoa.

Lakini kwa case ya Paka mweusi tayari ameshanasa kwene mtego wa kuwa na mabinti watatu, lkn kila mmoja anaona kasora kwake.
Kwa maana ingine akili yake imefika mwisho ktk kuamua yupi mke.

Sasa kwa sababu ndoa ni taasisi nyeti sana, hana budi kumwomba Mungu msamaha kwa kukosea kuwaweka wadada kwenye quee, then amuombe ampe mke mwema.

Kama yupo katika hao na iwe, kama hayupo, na apewe mke wake.

Au paka Mweusi we unasema je baba???
 
Preta

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
24,310
2,000
ila na wewe ni kiwembe.....watatu kwa wakati mmoja na wote unawagawia uroda.......duh....mi naona uchukue huyo mlupo kwa sababu mna katabia kanaendana.....atacover nafasi za hao wengine
 
Babuyao

JF-Expert Member
Jun 6, 2009
1,736
1,500
chagua kwa kuangalia positive elements za kila mmoja. Approach yako ya kuangalia makasoro ni approach ambayo haitakupa jibu sahihi kwani hakuna mwanadamu asiye na kasoro. Ila pamoja na kasoro zao tunavutwa na mengi sana waliyojaliwa na Mungu, na hasa upendo, uvumilivu, usikivu, upole, nk. kwa kutaja machache.
 
St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,401
2,000
ila na wewe ni kiwembe.....watatu kwa wakati mmoja na wote unawagawia uroda.......duh....mi naona uchukue huyo mlupo kwa sababu mna katabia kanaendana.....atacover nafasi za hao wengineAsante mama kwa comment yako,ila ukweli ni kuwa sija do na hata mmoja,ni zile date to za kimagharibi na kukaribisha mtu nyumbani kupata coffee.Nazingatia nadhiri yangu ya kuto do mpaka baada ya ndoa.
 
St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,401
2,000
chagua kwa kuangalia positive elements za kila mmoja. Approach yako ya kuangalia makasoro ni approach ambayo haitakupa jibu sahihi kwani hakuna mwanadamu asiye na kasoro. Ila pamoja na kasoro zao tunavutwa na mengi sana waliyojaliwa na Mungu, na hasa upendo, uvumilivu, usikivu, upole, nk. kwa kutaja machache.Babuyao kasoro hizo za hawa wachumba wewe unazionaje?
 
Mapinduzi

JF-Expert Member
Aug 23, 2008
2,424
0
Mungu hajawahi kusema tuwe na wachumba wangapi AMA, ila Mungu anatoa mke au mume, uchumba ni hatua ya kufikia kwenye ndoa.

Lakini kwa case ya Paka mweusi tayari ameshanasa kwene mtego wa kuwa na mabinti watatu, lkn kila mmoja anaona kasora kwake.
Kwa maana ingine akili yake imefika mwisho ktk kuamua yupi mke.

Sasa kwa sababu ndoa ni taasisi nyeti sana, hana budi kumwomba Mungu msamaha kwa kukosea kuwaweka wadada kwenye quee, then amuombe ampe mke mwema.

Kama yupo katika hao na iwe, kama hayupo, na apewe mke wake.

Au paka Mweusi we unasema je baba???

Basi mwambie paka mweusi aache kuchakachua wasichana kisaikologia kama sio kimwili kwa kigezo cha kutafuta mchumba.

Kama Mungu amempa kila mmoja wetu mwenza, na tutulie, tusubiri ufunuo.
 
Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,342
2,000
Natamani nikujibu..nakosa neno la busara la kukupa na lifti inaniacha!
Kwa sasa nakushauri tu,
Muombe Mungu ndugu yangu.
Kama umeona makosa zaidi ya mema nadhani wote hawakufai...tafuta mwingine!
au..
kuna weakness unayoona ni afadhali kwako!??
kesho nitahakikisha ninatafuta jhii thread nikupe stori yangu japo kwa ufupi...maybe itakusaidia.
Barikiwa.
 
LD

JF-Expert Member
Aug 19, 2010
3,015
2,000
Babuyao kasoro hizo za hawa wachumba wewe unazionaje?

mmmmh paka M unataka mke kweli wewe?? ushaona kasoro still unataka,
Tukushauri uingie na kasoro kwenye ndoa,

Shauri yako, hutakiwi kuona kasoro kwa mtu unaetaka kumuoa, na ukiiona haikupi shida ila unatafuta
njia ya kupambana nayo. "Upendo huficha mabaya yote."
 
LD

JF-Expert Member
Aug 19, 2010
3,015
2,000
Basi mwambie paka mweusi aache kuchakachua wasichana kisaikologia kama sio kimwili kwa kigezo cha kutafuta mchumba.

Kama Mungu amempa kila mmoja wetu mwenza, na tutulie, tusubiri ufunuo.

Ama, hicho ndo cha msingi, lakini Paka Mweusi kakosea kama mm na ww tunavyokosea,
lakini bado anayo nafasi ya kuchagua kuingia na kasoro kwenye ndoa, au kurudi kwa Mungu ampe Mke.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom