Wachumba/Wandaoa Wenye Nguvu

Said Cosmetics

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
2,001
1,586
"Strong Couple"
(Wachumba/Wandaoa Wenye Nguvu)

Niliwahi soma post moja Facebook iliyoandikwa na Kaka "Justine Malili" yeye aliandika kuwa;-

"Hutakiwi kumwambia mwanaume naomba tufunge ndoa, Bali muonyeshe ni kwanini anatakiwa kukuoa"
Ni moja ya post Kali kwa "Justine Malili".

Kupata mtu sahihi wa kuambata nae katika Magumu,Majalibu au hata kwenye furaha. Lazima pia Usahihi huanze ndani yako kabla hujampata mtu sahihi huyo.

Mr Robert Kiyosaki Na mkewe Kim Kiyosaki ni moja ya couple ninayoikubali sana kwani najifunza mengi kupitia couple hii. Achana Hizi Couple zenu za kuweka hadharani Siri za uchumba/ ndoa kwenye mitandao.

Mr.Kiyosaki alikua na maono makubwa sana, kutokana alipata mtu sahihi na yeye Usahihi ulianzia ndani yake. Akaweza kumuambukiza mkewe "Kimy Kiyosaki".

Na leo hii ni watu wanaofahamika sana duniani kama ni Wajasiliamali na Matajiri wakubwa ile hali walitokea chini kabisa. Walianza chini pamoja na kupanda juu pamoja.

Marehemu Dr.Mitimingi aliwahi kusema "Mafanikio ya mwanaume yatategemea na aina ya msichana aliyenae, ila mafanikio ya mwanamke hayatategemea ni aina gani ya mvulana aliyenae"

Kuna Wanaume wapo katika mahusiano na wasichana ambao ni "Very Positive" ila kutokana kukosa uwezo wa kumtazama msichana kwa jicho la tatu na hii kwasababu ya kuwa na mahitaji sana ya Ngono kuliko mapenzi. Wanajikuta wanaingia katoka shimo BOVU.

Ni vema kuwa na msichana ambaye ataniweka katika mazingira ya kunifanya niwe na "Meditation" (Kutafakari) kuliko kunilemaza na matumizi mazuri ya mwili wake.(Think)

Msichana "Smart" atakupa changamoto zenye kuleta "Strong Success".
Msichana wenye kuleta hamasa itakayo muhamsha mwanaume kutoka kwenye usingizi si msichana wa kawaida huyu.

Wanaume wakati tukiwa bize kutazama MAKALIO, SURA, UMBO na Miguu yao kwa macho mawili. Pia tumia jicho la tatu kutazama "MENTAL ATTITUDE" ya msichana.

Wasichana wana nguvu sana na madini kama wakijitumia na tukiwatumia kwa ufasaha.
 
Back
Top Bottom