Wachukuliwe Hatua za Kisheria

Wachukuliwe Hatua za Kisheria

La Quica

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
1,352
Reaction score
3,174
Habari wana jamvi, natumaini mko poa na wengine tukiendelea na mfungo wa pili.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Kumekuwa na wimbi la videos/video clips zikisambaa saba kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp, Instagram, Facebook, YouTube na kwingineko zinazoonyesha watu mbali mbali wa media zinajulikana na zile zisizojulikana ambazo nyingi ni channel za youtube zikirekodi watu na kuwauliza maswali ambayo wanajua kabisa hawataweza kujibiwa kifasaha hivyo kuifanya kama njia ya kujiingizia kipato kwa kuwachekesha watu.

Mfano kuna clip moja jamaa anamhoji mzee mmoja na mwisho anamwambia aseme "usisahau ku subscribe kwenye channel yetu" kitu ambacho anajua kabisa yule mzee hawezi kusema. Huu ni udhalilishaji wa hadharani na wahusika hawa wanatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kuna nyingine reporter wa channel fulani ameenda maeneo ya kijijini akaanza kuhoji watu kuwa "nini mtazamo wao baada ya shilole kuwa waziri". Kweli tunatumia uhuru wetu vibaya kwa kuwadhalilisha watu ambao hata huyo shilole hawajawahi kumsikia lakini kwa aibu tu anakubali kutoa maoni kumbe mnamkejeli tu.

Sio hizo channel tu, kuna watu binafsi pia wana record kwa simu na camera zao matukio yasiyokuwa na maadili na yakidhalilishaji au ya kikatili haya yanayohusisha watoto wadogo.

Mfano leo nimeona clip ya mwalimu akiwa anamlazimisha mwanafunzi asome kitabu chenye picha na majina ya kitu kilichochorwa kwenye picha. Ukiangalia hiyo video ni unyanyasaji mtupu kwakuwa mwanafunzi anakosea lakini mwalimu badala ya kumsahihisha anamrekodi na kuendelea kumshurutisha aendelee kusoma. Hivi waalimu mmefundishwa kweli maadili ya kazi? Au ni wachache wasiojielewa wanafanya masuala ya kinyanyasaji kwa watoto?

Nashauri wale makamanda wa polisi wanaofatilia masuala ya hovyo kama mtu kujichora tattoo au mtu kuguma anapopisha na mwanamke aliejazia sasa waachane na hayo masuala na kuangalia upande huu ambao kiukweli unakera na kudhalilisha watoto wadogo na wazee wetu ambao kutokana na kutokuwa na kasi ya kitechnolojia wapo nyuma sana na hivyo kutojua mambo mengi.

Kutokujua kwao mambo kusiwafanye nyie vijana kuwafanyia mzaha na kuwadhalilisha wazee wetu kwenye mitandao kwa kuwageuza vitegauchumi kupata pesa kwa kuongeza viewers.

Serikali ipige vita tabia hizi. Kuna mambo mengi yakufanya kujiingizia kipato ila sio udhalilishaji huu wa watoto na wazee wetu. Nawasilisha
 
Naunga mkono hoja ya mtoa mada,, kudhalilisha watu tena waliokuzidi umri sio ubunifu kabisa.
 
Back
Top Bottom