Wachina walitumia kondom za utumbo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
120928190017_condom_pig_304x171_internet_nocredit.jpg


Kondom ya Utumbo wa Nguruwe

Nani asiyejua Kondom?

Kondom ya Utumbo wa Nguruwe

Nani asiyejua kazi ya Kondom?

Lakini unajua kifaa hicho ambacho siku hizo husambazwa bure kilianza lini na wapi?

Tarehe yenyewe haifahamiki lakini katika karne ya 15 yaani miaka mia 6 iliyopita kondom zilikuwepo na

zilikuwqa zinatumika katika bara la Asia.

Miaka mia sita iliyopita Kondom nchini china zilikuwa nizatengenezwa kutumia utumbo au mbuzi au kondoo.

Matajiri walikuwa wakitumia Kondom zilizotengenezwa kwa karatasi ya hariri iliyopakwa mafuta.

Nako nchini Japan Kondom zilikuwa zikitengenezwa kwa magamba ya kobe au pembe za wanyama . Naama

pembe ilikuwa ikivaliwa kama kondom..ni huko Japan, miaka mia 6 iliyopita.

Ni katiuka karne iliyopita , mwaka 1900 kondom zilizotengenezwa kwa utumbo wa mbuzi na kondoo hata

utumbo wa ngombe zilianza kuenea duniani.

Enzi hizo ilikuwa inatumiwa kukinga magonjwa ya zinaa na kuzuia mimbia isiyotakikana.
.........

Ni kawaida kwa wanawake wengi wakati wa ujazito kuanza kutapika , kuwa ni kichefu chefu ,kuhisi kisunzi au

kizunguzungu , kujisikia mnyonge, hasa wakati wa asubuhi. Wazungu wanasema ni Morning sickness.

Wataalam wanasema haina sababu moja. Lakini wanakubali kuwa husababishwa na ongezeko la homoni hasa

ya Estrogen katika mwili wa mwanamkea ambayo inaweza kumuongezea , uwezo wa kusikia harufu hasa

mbaya. Kuongezeka kwa maji aina ya gastroline.

Na unafahamu kuwa mwanamume.Baba mwenye nyumba pia anaweza kuwa na dalili hizo hizo za ujauzito

yaani ?, kizunguzungu,kutapika , kichef chefu , tumbo kufura na kuwa na hasira kama mkewe?

Kwa wakati huu Mike Dowdall , bwana mwenye umri wa miaka 25 kutoka Manchester Uingereza amefura

tumbo, anatapika tapika , asubuhi, husikia kisunzi au kizunguzungu na anapenda kula vitu vichachu kama maembe mabichi yalitiwa chumvi au pilipili.

Kwa wakati huu mpenzi wake Amanda Bennett ni mjamzito. Dahili za Mike zilipoanza bi Amanada alichukulia

kwamba mpenzi wake ambaye wameishia naye miaka mitatu anamfanyia mzaha au stihizai Eti anamuiga vile anavyo tapika, na kupenda kula kula.

Lakini madaktari kutoka Manchster wanasema Bwana Mike ana ugonjwa wa mimba bandia. Wao wanaita Couvade syndrome

huu sio uchawi , bali ni ugonjwa unaoweza kuwapata wanaume. Tumbo kufura, kutapika tapika asubuhi, kuhisi kizunguzungu na kupenda kula maembe ya liotiwa chumvi au pilipili.

Mike amekuwa na uja uzito bandia kwa wiki 33 na kama vile tu akina mama walio na mimba , Mike ameongeza uzani au zaidi ya kila 3 na sasa anajihisi mchovu kila mara, kuumwa na mgongo na kwnda haja ndogo kila mara.

Madaktari hao wanasema ugonjwa huu unaweza kusababishwa na ile hali kuwa wasiwasi unaposubiri mkeo kujifungua, au pia kuwa karibu sana na mkeo.

Bi Amanda ambaye ana mimba ya wiki zaidi ya 34 sasa analazimika kumsugua mumewe mgongoni na kiunoni kila siku na kumkanda tumbo lake.

Habari hizo zimeshamiri katika gazeti la The Sun la uingereza. BBC Swahili - Medianuai - Wachina walitumia kondom za utumbo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom