Hii stori imepindwa ili kuchochea chuki dhidi ya Wachina. Impression niliyoipata nilidhani labda Wachina wameenda kupiga kambi kwenye hifadhi fulani ya misitu na kuanza kuvuna kinyume cha sheria, kumbe not even close. Wao wanamiliki viwanda, na kumiliki kiwanda sio kosa wala kununua malighafi sio kosa. Tuache kuwanyanyasa na kuwasakama raia wa kigeni bila sababu za msingi. Hii haitotusaidia.
Awali ya yote hivi kuna ubaya gani wananchi wakauza rasilimali zao kama mazao ya shamba au miti? Serikali najua haikuwasaidia kwa lolote hivyo isijitie kimbelembele eti kulinda mazingira. Kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake, sasa wananchi huko walipo hawana njia nyingine ya kutokea, maana mmeshindwa kuwaongoza kuelekea tunu ya maendeleo.