Majoja
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 612
- 186
Wachina wawili nimekuta wakijiuguza majeraha huku wamekaa chini barabara ya Sam Nujoma karibu na Cocacola baada ya kula kipigo toka kwa wananchi wenye hasira kali.
Kutaonana na tabia iliyokithiri ya wenzetu wachina kujichukulia sheria mkononi inasemekana walimpiga hadi kuzirai kijana mmoja ambaye inaelekea aliwafanyia uhuni au kuwaibia, sehemu za Mwenge, Majembe Auction Mart.
Wananchi na watu waliokuwa karibu walijibu mapigo kwa kuanza kuwarushia mawe.Hawa jama wa Kichina wakaliacha gari lao lilokuwa na mbao na walijaribu kukimbia kuelekea Cocacola lakini ndio kundi la watu lilivyoendelea kuwa kubwa na mawe kuongezeka.
Wachina hao ambao inasemekana wanamiliki kiwanda cha mbao sehemu za Mikocheni maarufu kama "Kwa Mpemba Osama" nimewakuta wamekaa chini wakisubiri polisi.
Hata hivyo vile vile inasemekana kisago alichopewa kijana laiyetaka kuwaibia kilikuwa ni kikubwa na kijana kaumia vibaya sana.