Wachina ni wezi

Rais wao na Rais wetu walisaini mikataba.Kabla ya kuhoji Wachina wanafanya nini au wamebeba nini ni vyema kuuliza kama unaweza kupatiwa kopi ya mikataba hiyo. Na kwa kuwa huwezi kupewa ama kujua chochote kilichopo kwenye mikataba hiyo ni vyema tu kuendelea na shughuli zako za maendeleo............
 
Mkuu wakati mwingine ni vizuri ukawasikiliza watanzaia wenzako ambao wana walao ujuzi wa kiufundi katika nyanja hizi za mafuta na gezi, mtu umefafanuliwa kwamba si rahisi mwekezaji yeyote kuweka mitambo na infrastructure za kichimba mafuta na gezi bila ya kuonekana, narudia kusema visima vya kuchimba mafuta na gesi havina kificho. Hii tabia ya baadhi ya Watanzania wenzetu kudhani kila mwekezaji ni mwizi yatakuja kututokea puani, wawekezaji watatuachilia mbali tuendelee kukalia uchumi na umaskini wetu kwa kujitia jeuri huku tukijua wazi kwamba Mitaji ya kufa mtu hatuna, hata tukikimbilia Mabenki ya kimataifa yenye uwezo hayawezi kutoa pesa kwa nchi ambayo aina ujuzi wowote katika nyanja za uchimbaji mafuta na gezi, hatuna credibility yoyote kiufundi/kitaalamu katika nyanja hizi. Tukea tukijua kwamba kuna nchi nyingi za Kiafrica zenye kiu ya maendeleo, wanakaribisha wawekezaji kwa mikono miwili alafu wanawekeana mikataba ya win win situation sisi tunabaki kulalama kwamba wamepania kutuhibia, wakati wenye matatizo ni sisi na ufisadi wetu wa kukosa uzalendo - hapa tunajitia kulahumu wageni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…