Wachina ni wezi

Mapambano Yetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
1,133
Reaction score
2,128
Kuna meli kubwa sana za wachina zinakuja Mtwara na zinashusha mitambo yenye mashaka miongoni mwa watanzania. mbali na mitambo hiyo, kunatetesi kuwa meli hizo zinaiba mafuta eneo la mtwara. ndani ya meli hizo hakuna mtanzania/mwafrika anayeruhusiwa kuingia ndani (hata maofisa usalama). ni wachina pekee na wenye vibari ndio wanaoingia kwenye meli hizo. watanzania tuwe makini na ujio wa watu hawa kwani kuuza mapambo ni geresha ya kutulaghai. nyuma ya hilo (mapambo) kuna mambo makubwa yanaendelea.
 
Wanaoruhusiwa kuingia ni kina nani........?
 
Wameishauziwa nchi hao kwa mikataba waiosainishana huko china ili kujikomboa fanyauamuzi sahihi 2015 ili tuirudishe nchi kwa Wanzania na tuwahukumu hawa waliotuuza bila kutufahamisha.
 
Je, Berry white, na Shilling mkubwa wanaruhusiwa kuingia?
 
Mkuu mbona Taifa letu alijawahi kuvumbua mafuta, tuna gesi kama sikosei!! Sasa hao wachina walianza lini kuchimba na kuhiba mafuta, kitu kingine kuna tofauti kubwa kati ya meli za kubebea mafuta/gesi na meli za kubeba mizigo ya kawaida mfano mabomba ya kusafirishia gesi kuja Dar na mitambo ya kuhunganisha mabomba na vifaa vya ujenzi wa nyumba za kuweka pump za kusukumia gesi. Mkuu si rahisi Wachina kuiba chochote bila ya kujulikana especially MAFUTA na GESI.
 
Wachina, wazungu, waarabu wote sawa tu. Ukikaa sawa au ukijipendekeza lazima wakulize.
 
Mikata 19 ya siri alisaini mkuu wako,,,sasa unataka ujue kinachoendelea?
 

nakushauri uongeze upeo wa kufikiri, tangu lini mwizi akaja openly? kama ni wanakuja kwa wema ni kwa nini hawaruhusu ukaguzi wa meli zao? mitambo inayoletwa ni kwa nini iletwe kwa uficho? kwa taarifa yako wachina wana agenda ya siri na tanzania na mikataba wanayopewa itatutokea puani. wamesaini mikataba ya kurekebisha na kujenga miundombinu za kijeshi, cha ajabu wakati wa ujenzi wa sehem muhim za miundombinu hakuna mtanzania anayeruhusiwa kuwepo wala kukagua kinachoendelea. je? tutapona kwa stairi hii kweli.
 
Mkuu mimi sikutaka kuingia kiundani kuhusu masuala haya - kwa kifupi ni kwamba hakuna binadamu anaweza kuchimba/ kusafirisha CRUDE OIL bila ya kujulikana. Kwanza rigs za kuchimbia mafuta/Gesi zinajengwa hadi kufikia urefu wa ghorofa nane hadi kumi, rigs hizo azina kivicho zinanekana hata ukiwa umbali wa maili thelathini na ushee - sasa mkuu hapo wizi unawezaje kufanyika bila ya kushtukiwa. Kitu kingine hivi mkuu unategemea jeshi linaweza kweli kuweka miundo mbinu yake adhalani??
 
Nachofahamu ni kwamba hayo mafuta yameshaanza kuchimbwa siku nyingi sana. Wanachokifanya hao waChina ni muendelezo wa ku-prove kuwa sisi waTZ ni mazezeta/mazuzuri, watu tusiokuwa na uchungu na nchi yetu...

Shame on YOU mTZ...
 
Ahhh! mambo ya nchi hii bana, huwa yanakera sana wajameni!
 


kama Inafikia Hatua hata viongozi wa jeshi hawaruhusiwi kufika kwenye baadhi ya miundombinu inayojengwa mpaka ujenzi ukamilike tutawaaminije watu hawa? tunauhakika gani kuwa hawawez kuweka mabom na mitego mingine kwa manufaa yao ya baadae? kuhusu swala la mafuta hilo ukubali usikubali watanzania tunaliwa.
 
Mikataba iliyosainiwa kisiri ndio kiini macho. Watasema wanafanya utafiti wa mafuta kumbe wanachimba mafuta. Watasema wanafanya uatafiti wa madini kumbe wanabeba madini mchanan na usiku. La msing ni kuwa viongozi wakuu wa nchi wanajua kinachoendelea na ten percent zao zinaingizwa mabenki ya nje. Katiba mpya ndio ingekuwa suluhisho lakini ndio hivyo tena imeshadakwa juu kwa juu.
Ushauri wangu: Tumwombe Mungu kwa dhati kuwa alitupa nchi hii na mali zote zilizopo ili tuzimiliki na kuzifaidi sisi. Tunaomba atuondolee viongozi wote wabadhirifu pamoja na wageni wote wezi wa mali yetu. Amina.
 

Acha uoga, shirikiana nao vizuri. Mafuta sio maji kunyonywa kirahisi hivyo! Watu wako baharini mwaka wa 10 sasa hawajanyonya hata lita 1. Hakuna mwekezaji wa maana duniani kama mchina, wengine watakupa neti uzuie mbu wasikuume hawatakupa sumu ya kuua mbu, watakupa mahindi ukiwa na njaa, ila hawakotayari kukupa jembe la kisasa ulime mahindi mwenyewe wala angalau hata kujenga hicho kiwanda cha net ili tutumie pamba yetu kuzitengeneza. Japo kila mfanya biashara shida yake ni kutengeneza faida kubwa lakini Fuatilia sana utagundua mchina anafanya makubwa na yuko tayari kujenga vitu vya kudumu kupambana na tatizo sugu la umasikini ukilinganisha na wezi wa magharibi.

Cha muhimu tu ni kuhakikisha hatusaini mikataba isiyo na maslahi
 
CCM wanalala uchi wa mnyama kitanda kimoja na Mchina unategemea nini???

Chama tawala kikipigwa mjengwa wa akili nchi nayo pia inabakwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…