Wachina kufukuzwa kariakoo

Shytown

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2025
Posts
468
Reaction score
791
Binafsi nafikiri kuna changamoto watu hawajaziangalia vizuri kabla ya kufikiri kuwa wachina ni tatizo nalo ni ukosefu wa Elimu, Elimu, Elimu ya Biashara
1. Wafanyabiashara wa Tanzania walio wengi hawana Elimu ya biashara
2. wafanya biashara walio wengi ni wabinafsi
3. baadhi ya wafanya biashara wanakwepa kodi

Nifafanue kidogo
1. Kwa kuwa wafanya biashara wetu walio wengi hawana Elimu ya Biashara, ananunua meza china shs 35,000 anakuja hapa anauza 120,000 (Wizi mtupu)
Mchina akinunua meza hiyo hiyo china kwa shs 35,000 akipiga gharana za manunuzi, + usafirishaji + kodi ya serikali+ gharama za uendeshaji akaweka na faida yake 20% bei ikawa 95,000; mnasema anakiwanda china; sijui anamtaji nk nk lakini ninavyo ona tatizo ni Elimu, Elimu, Elimu ....na tamaa ya wabongo ya kuwanyonya watanganyika ili mzidi kutajirika....
Yaani mtu anunue kiatu china shs 22,000 akija hapa anakuambia tu shs75,000 bila aibu; eti maongezi yapo??? hata ukimuambia amepataje hiyo bei hajui?
Wafanyabiashara hawawataki wachina kwa sababu ya tamaa ya kutaka kuuza ghali na kujitajirisha bila kujua wanawanyonya WATANGANYIKA...
UKWELI NI KUWA, KODI YA SERIKALI KWENYE LILE SOKO INAWEZA KUONGEZEKA MARAMBILI + KAMATUTAWARUHUSU WACHINA WAFANYE BIASHARA KWA UHURU KWANI TUTAWAVUTIA WAFANYA BIASHARA WENGI WA NCHI JIRANI....
 
Hao wachina unao wapamba ndio wakwepa kodi konkodi, wana shirikiana na viongozi wenu uchwara ili kukandamiza mazingira ya biashara kwa wazawa.

Mchina ana leta mali, hapigwi kodi ya bandarini, kodi ya tra ina lipwa kwa kiongozi kwa kumkadiria.

Wana pewa mikopo pale bot with a nonsesical interest as a return, hakuna anaye hoji

Halafu una kuja kuropoka nonsense
 
Mbona pale KARIAKOO, wabongo wakisikia tu TRA wameanza kukagua maduka (walipa kodi) wanafunga na kuyaacha maduka ya wachina ndio yanabaki wazi?
Nyie mnaolipa kodi vizuri kwa nini mnafunga na kutokomea?
 
Mbona pale KARIAKOO, wabongo wakisikia tu TRA wameanza kukagua maduka (walipa kodi) wanafunga na kuyaacha maduka ya wachina ndio yanabaki wazi na wanakaguliwa wanakutwa wapo sawa?
Nyie mnaolipa kodi vizuri kwa nini mnafunga?
Maduka yote huwa yana fungwa?, njoo na evidence tuone.
 
kwa jinsi kodi ilivyo sio fair ikiwa hakuna konakona bidhaa zitakuwa bei juu sana
 
hizi ni akili zinazo waza ndagu na kwenda kwa babu, ndio zinataka kubaki Kariakoo mmeshindwa kushindana na wachina.

Kuhusu kodi hata watanzania ni wakwepaji sugu, utauziwa bidhaa bila risiti na ukikazia watakukomoa kwa kukupandishia bei wakati bei wanayokuuzia bila risiti ni ile yenye kodi

Wateja wanachojali ni unafuu, heri niende kw mchina kwa bei nafuu kwa kitu kile kile ambacho mbongo anataka kunitandika bei kubwa kwa tamaa iliyokithiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…