Wachimbaji wadogo hatarini kufa kwa zebaki

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,565
21,558
mercury_01-300x240.jpg


UTAFITI unaonyesha kuwa asilimia kubwa ya wachimbaji wadogo wanaochenjua madini ya dhahabu kwa kutumia kemikali ya zebaki, wako hatarini kupoteza maisha kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha kemikali hiyo mwilini.

Hayo yalibainisha katika semina ya jinsia na maendeleo (GDSS) iliyoandaliwa na Mtandao ya Kijinsia Tanzania (TGNP) na Meneja Programu wa Asasi isiyo ya kiserikali – AGENDA, Silvani Mng’aya.

Mng’aya alisema utafiti huo wa mwaka 2013 ulifanywa kwa watu wanaofanya kazi na kuishi karibu na migodi, ikiwa ni pamoja na wachimbaji wadogo katika maeneo ya Matundasi na Makongolosi, Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

“AGENDA ilifanya utafiti wa kutumia nywele kwa watu 200 ambao ni wachimbaji wadogo na watu wanaoishi karibu na maeneo hayo. Theluthi ya waliopimwa walikutwa na viwango vya juu vya zebaki,” alisema Mng’aya.

Alisema kuwa kiwango cha zebaki mwilini kilichowekwa na Mamlaka ya Uhifadhi Mazingira Marekani (US Environmental Protection Agency) ni sehemu moja ya milioni (1ppm), lakini wapo ambao ilifika kiwango cha sehemu 236 ya milioni (236 ppm).

Pia alisema kwa mujibu wa utafiti kwa washiriki 56 kutoka nchi 40 katika mkutano wa kwanza wa wadau kujadili kuanzishwa kwa mkataba wa kimataifa wa kudhibiti zebaki uliofanyika Stockholm nchini Sweden mwaka 2010, viongozi wengi kutoka nchi za Afrika walikutwa na kiwango kikubwa cha zebaki ukilinganisha na mataifa yaliyoendelea.


Chanzo: Mtanzania
 
Back
Top Bottom