Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 780
- 1,831
Jumla ya wachimbaji wadogo 25 kutoka katika mgodi mdogo wa Nyandolwa unaomilikiwa na kikundi cha Wachapa Kazi, uliopo kijiji cha Mwongozo Halmashauri ya Shinyanga, wamefukiwa na kifusi baada ya mgodi kutitia.
shughuli ya uokoaji imefanywa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wachimbaji katika eneo hilo, na tayari wachimbaji wawili wameokolewa.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro amesema kuwa wachimbaji hao walikuwa katika mashimo matatu tofauti, ikiwemo shimo la duara namba 106 lenye watu 6, 103 lenye watu 11, na duara namba 20 lenye watu 8. Juhudi za uokoaji zinaendelea.
Soma Pia: Shinyanga: Watu sita wafariki dunia kwa kufukiwa na kifusi mgodini 11 waokolea
Tukio la kutitia kwa mgodi huo limetokea Agosti 11, 2025 saa nne asubuhi, wakati shughuli za matengenezo ya maduara hayo zikiendelea.
Mtatiro amewasihi wachimbaji kuwa watulivu wakati jitihada za kuokoa uhai wa walioko chini zikiendelea
Azam TV

so sad yote hayo kisa umaskin