Wachezaji wanne Simba kutolewa kwa mkopo

Nov 23, 2017
42
98
Wachezaji wanne Simba kutolewa kwa mkopo

Bamwanga Blog

Upana wa kikosi cha Simba kwa sasa umefanya baadhi ya wachezaji kukosa namba kikosi cha kwanza, Kocha Mkuu Patrick Aussems anataka kuwatoa wachezaji wanne kwa mkopo.

Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa kwa sasa mpango wa kusajili dirisha dogo ni kwa nafasi mbili tu ambazo zimeelekezwa na kocha ila ametoa maagizo pia ya kutoa wachezaji wanne kwa mkopo.

"Kocha anataka kuwatoa wachezaji wanne kwa mkopo ili waweze kupata nafasi katika timu watakazokwenda kutokana na ugumu wa kupata namba jinsi ulivyo ndani ya kikosi chetu kwa sasa.

"Suala la wachezaji gani hilo bado hajaliweka mezani anatarajiwa kutoa ripoti ya majina ya wachezaji hao ambao watatolewa kwa mkopo hivi karibuni," kilieleza chanzo.

Tayari kuna timu ambazo zimetuma barua kuwaomba wachezaji kwa mkopo kutoka Simba ikiwa ni pamoja na African Lyon, Singida United na wachezaji wanaowaniwa sana ni Marcel Kaheza, Rashid Juma, Nicholus Gyan na Mohamed Rashid.

Bamwanga Jr
 
Back
Top Bottom