DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Kuelekea mchezo wa michuano ya CHAN kati ya Taifa Stars dhidi ya Morocco utakaochezwa leo Agosti 22, 2025 katillka dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam, Mkuu wa mkoa huo Mhe. Albert Chalamila ametangaza zawadi na motisha zitakazotolewa na uongozi wa mkoa kwa kishirikiana na wadau mbalimbali ili kuchochea ushindi katika mchezo huo.
Zawadi hizo ni pamoja na kitita cha shilingi za kitanzania milioni ishirini zitakazotolewa kabla ya mchezo huo, zawadi ya shilingi milioni tano kwa kila goli, shilingi milioni moja kwa kila mfungaji wa goli huku atakayetoa pasi ya mwisho kuelekea goli (assist) atazawadiwa shilingi laki tano.
Kwa upande wa mlinda mlango (Goalkeeper) katika mchezo huo atazawadiwa gari aina ya toyota crown endapo mchezo huo utamalizika bila kufungwa goli lolote.