Tuwekee mchanganuo wa mapato na matumizi ya hizi club halafu utuambie kama kweli mapato yao yanatosha kuendesha hizi club kama unavyotaka. Mechi zinazoingiza Tshs 200 million ni kati ya watani wa jadi na sidhani kama mechi kama ya Simba na Polisi Dodoma inaweza kuingiza kiasi hicho.
Ajali aliyopata mchezaji wa Simba haikutokana na ubovu wa gari. Ajali ni ajali hata gari mpya inaweza kupata ajali.
Hizi kasumba za kuona Keko, Temeke, Mbagala sio sehemu nzuri za kuishi ni mbaya sana.