Wacharazwa viboko 15, baada ya kukutwa wakiwa na watoto bar

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,911
2,891
Wanawake wawili wakazi wa Sanya mkoani Kilimanjaro wamechapwa viboko 15 kila mmoja na kulipa faini ya shs 50,000 kama adhabu baada ya watu hao kufanya kosa la kuwapeleka bar watoto wenye umri chini ya miaka 18.

Jambo hilo ni kinyume na sheria ndogondogo ambazo wanakijiji hao wamejiwekea. nadhani kama sheria hii ingepitishwa kwa nchi nzima ingesaidia kupunguza unywaji pombe holela.
 
wanawake wawili wakazi wa sanya mkoani kilimanjaro wamechapwa viboko 15 kila mmoja na kulipa faini ya shs 50000 kama adhabu baada ya watu hao kufanya kosa la kuwapeleka bar watoto wenye umri chini ya miaka 18 jambo ambalo ni kinyume na sheria ndogondogo ambazo wanakijiji hao wamejiwekea. nadhani kama sheria hii ingepitishwa kwa nchi nzima ingesaidia kupunguza unywaji pombe holela.
Safi sana.Kilimanjaro unywaji pombe ni tatizo .Kreti moja ya soda unakuta kijana mmoja mkubwa hawezi kubeba unakuta vijana wakubwa wanne wanasaidiana kubeba kreti moja ya soda na bado wanayumba yumba.

Yaani mkoa wa kilimanjaro unabidi upambane kwa nguvu zote na tatizo la ulevi
 
Akina mama, wanafunzwa kulea watoto wao kwa viboko!!! Kweli gia zimebadilishiwa hewani
 
Nakumbuka hiyo ishu iliandikwa gazetini. Naona sasa wanamaanisha katika kuitekeleza kwa vitendo.
 
Safi sana.Kilimanjaro unywaji pombe ni tatizo .Kreti moja ya soda unakuta kijana mmoja mkubwa hawezi kubeba unakuta vijana wakubwa wanne wanasaidiana kubeba kreti moja ya soda na bado wanayumba yumba.

Yaani mkoa wa kilimanjaro unabidi upambane kwa nguvu zote na tatizo la ulevi
We jamaa ni muongo sana aisee
 
Sidhani kama sheria ya nchi inaruhusu corporal punishment!
Kuna sheria ndogo (bylaws) ambazo hutungwa na mamlaka husika kama hiyo ya kijiji na zinakubalika sababu mchakato unaruhusiwa kikatiba. Wamekosea sana kupeleka watoto baa. Pia kuna wale ambao hutuma watoto sigara na pombe, tabia mbaya sana hiyo.
 
..hahahaa sanya juu ndipo ninapoishi..acha wachapwe tu ! ni sheria zao walizojiwekea wenyewe wananchi kama kijiji.
 
sheria hairuhusu watoto chini ya 18 kuwa bar ukiwa unachangia kitu uwe unafikiria na utafakari eti za wana kijiji
nonesense
Nani kasema kwamba watoto chini ya miaka 18 wanaruhusiwa we mkurupukaji? Nimesema kwa wana kijiji kumchapa huyo mama inaweza
wageuka kama akiwashitaki...... hapo wapi kuna uhalali wa watt kupelekwa bar? Nimewahi ona sungu sungu wanashitakiwa mahakamani na makamasi yanawatoka maana walikipata cha
moto baada ya kumchapa mwalimu wetu
mmoja.... achana na bylaws za vijijini bana.....
 
Sijafurahishwa na tendo la kuwachapa viboko watu wazima. Kosa wamefanya lakini si kucharazana viboko. Faini ingetosha.
 
Hivi kwa mfano kama mtu mzima upo mahali ambapo ni ugenini na una mwanao ambaye umri wake ni chini ya umri wa miaka 18 na ikatokea mna njaa na hakuna sehemu nyingine wanakouza chakula zaidi ya bar iliyo jirani utafanyaje ili upate chakula wakati huo ukihakikisha usalama wa mtoto uliye nae?
 
Kuna sheria ndogo (bylaws) ambazo hutungwa na mamlaka husika kama hiyo ya kijiji na zinakubalika sababu mchakato unaruhusiwa kikatiba. Wamekosea sana kupeleka watoto baa. Pia kuna wale ambao hutuma watoto sigara na pombe, tabia mbaya sana hiyo.
By laws zinatakiwa zisipingane na sheria mama yaani katiba ya jamhuri ya muungano,katiba inakataza aina yoyote ya udhalilishaji na kuvunja utu wa mtu....Ndio maana kuna mchangiaji hapo juu amesema hawa wa mama wakienda mahakamani kuna uwezekano wa hao watu kukutwa nahatia...Watoto kwenda bar ni kosa kisheria but sio kuwachapa watu wazima...
 
Back
Top Bottom