Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,071
Kwa sasa kama kuna wanasiasa wasioleweka, wasioweza kuaminika au kukubalika popote, basi kundi la wabunge wa Covid 19 ndio kinara. Kisiasa ni kama wamechanganyikiwa hivi, hawajui pakushika na hawajui pakuacha, chochote kilichopo mbele yao chenye kutoa mwanga wa matumaini wa maisha yao ya kisiasa wanakikimbilia. Hapa ni mifano halisi ya namna wanavyoweweseka.
1. Baadhi yao walianza kujiambatanisha na harakati za Mbowe wakati ule akiwa anataka kutetea kiti cha uenyekiti wa Chadema, aliposhindwa wakatemana naye kimya kimya!
2. Wengine wakaamua kujiambatanisha na Lissu mara tu aliposhinda uenyekiti wa CHADEMA, Lissu alipoanza kukomaa na No Reform No Election wakapotelea mitini kimya kimya.
3. Wapo wengine wakaibukia kwenye lile genge la watia nia wa CHADEMA lililojipashika jina la G55, ngoma ilipokuwa ngumu kwa hilo kundi baada ya kusambaratishwa na CHADEMA nao wakapotelea mitini.
4. Wengine wakaibukia na harakati za CHAUMA, kelele za Chauma zilizopoanza kupoa na kusahaulika nao kimya kimya wakapotea kusikojulikana.
5. Wengine wakajipa matumaini ya kukimbilia kwa Zitto Kabwe kule ACT, nako wamekaa kimtego kimtego, wachache mnoo wamejiunga huko lakini ni kama hawaai kama kuna kutoboa. Dakika yoyote wanaweza kukiamsha.
6. Wengine bila aibu, wakaamua kuunga mkono juhudi, wamehamia CCM na bila kupima kina cha maji mbio mbio wamekimbilia kuchukua fomu za kuomba kugombea ubunge.