Wabunge wetu wa UKAWA wakitoka nje bungeni huenda wapi?

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
7,377
10,641
Ni mara kadhaa wabunge wetu wa upinzani huamua kutoka nje ya vikao baada ya kutofautiana na wenzao. Eitha hutoka kwa vurugu au kwa amani kama ilivyokuwa leo.

Sasa nataka kujua huwa wanaelekea wapi na je kale ka posho huwa wanachukua kote au nusu? Walau huyu wa kwetu huwa namuona anarudi ila sijapata muda wa kumuuliza huenda wapi akisusiaga vikao.

Tujulishane hapa ili tuone kama hizo shughuli wanazoziendea huwa zinajenga nchi au huwa ni za maslahi ya nani.
 
Ni mara kadhaa wabunge wetu wa upinzani huamua kutoka nje ya vikao baada ya kutofautiana na wenzao. Eitha hutoka kwa vurugu au kwa amani kama ilivyokuwa leo. Sasa nataka kujua huwa wanaelekea wapi na je kale ka posho huwa wanachukua kote au nusu? Walau huyu wa kwetu huwa namuona anarudi ila sijapata muda wa kumuuliza huenda wapi akisusiaga vikao. Tujulishane hapa ili tuone kama hizo shughuli wanazoziendea huwa zinajenga nchi au huwa ni za maslahi ya nani....

Wewe unawaza posho tu?
 
Wanaenda Chako ni Chako, pitia pale ukale bia na mbuzi za ofa kutoka kwa Waheshimiwa...!
 
Wanaenda mnadani kula nyama....wengine kwenye miadi na mishe za hapa na pale(rejea elimu ya hapa na pale ya kubenea)
 
Huwa wanaenda sehemu tofauti tofauti.
Wengine huenda bar kunywa na kucheza pool, Wengine wanaenda saluni (kwa wale wa viti mahalum), Wengine wanaenda kwenye vijiwe vya kahawa kupiga stori za hapa na pale .

Pia Wengine huenda UDOM kushangaa Shangaa magorofa na kusaka totozi.
 
Mbona nimeongea mengi? Mkuu nataka kujua tu kama ka kodi kangu wanakatafuna kihalali bila kusahau kupata uelewa wa kama kura yangu wanaitendea haki

Pole ndugu yangu kwa kuendekeza propaganda za kizee. Aliyekuambia bunge lina nguvu nchi hiii ni nani? Bunge kwa ujumla wake bila kujali wabunge wa upinzani wala wa ccm hawana chochote wanachoweza kuamua na serekali ikatekeleza zaidi ya maswali na majibu bila utekelezaji. Hebu niambie ni maazimio mangapi yamepitishwa na bunge na bado serekali haitekelezi ama inatekeleza inavyotaka. Ni budget ngapi zinapitishwa na bunge lakini utekelezaji wake ni tofauti na bunge lilivyopitisha? Kwa taarifa yako bunge ni eneo lingine la kula hela za wananchi bila faida japo lipo kisheria.
 
Ni mara kadhaa wabunge wetu wa upinzani huamua kutoka nje ya vikao baada ya kutofautiana na wenzao. Eitha hutoka kwa vurugu au kwa amani kama ilivyokuwa leo.

Sasa nataka kujua huwa wanaelekea wapi na je kale ka posho huwa wanachukua kote au nusu? Walau huyu wa kwetu huwa namuona anarudi ila sijapata muda wa kumuuliza huenda wapi akisusiaga vikao.

Tujulishane hapa ili tuone kama hizo shughuli wanazoziendea huwa zinajenga nchi au huwa ni za maslahi ya nani.
maswali mengine ni yakipuuzi sana. na hili ni moja wapo.
 
Back
Top Bottom