Wabunge wetu na wingi wa matatizo ya wananchi.

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Sherehe ya wabunge kujipongeza baada ya awamu ya tano kuanza kazi, baada ya rais kuwa ameshalihutubia bunge ilikuwa igharimu zaidi ya shilingi milioni 200. Rais akatoa maagizo itumike sio zaidi ya shilingi milioni 15 ili fedha nyingine iende kununulia vifaa vya muhimbili hospital.

Na fedha hiyo ya sherehe ilitolewa na mojawapo ya taasisi kubwa nchini. Katika mazingira ya kawaida hakuna ambaye angeweza kuhisi uwepo wa aina fulani ya ukaribu kati ya watoa fedha za sherehe na wahudhuriaji wa ghafla hiyo. Ni maisha yaliyokuwa ya kawaida kwa makampuni makubwa kuwa na "wema" kwa wabunge.

Na wabunge wetu wakiwa kwenye kamati zao husafiri ndani ya nje ya nchi, wakati mwingine kukagua ufanisi wa taasisi mbalimbali pamoja na kwenda kujifunza jinsi nchi nyingine zinavyosimamia maendeleo yao.

Hizi kashfa za rushwa zinazowakumba wabunge, zinatufanya tujiulize kuhusiana na ule "wema" wa makampuni kuchangia sherehe kama ile ambayo zaidi ya shilingi milioni 200 ilipangwa kutumika. Ni kama vile mtu anaununua upendo wa mtu mwingine, ili kesho ikifika mambo ya mnunuaji wa upendo yasije kuharibika.

"Scratch my back and I will scratch yours", huo msemo wa kimombo unafanana sana na mazingira haya ya wabunge kuwa watu muhimu sana kwa wakurugenzi wa taasisi kubwa nchini. Huu utamaduni wa kibepari wa watu kujenga mitandao mipana ya maslahi, haiwezi kuwa na faida kwa mwananchi wa kijijini ambaye analima katika mazingira duni, ambaye afya yake haina bima.

Ni matumaini yangu kuwa siku inakuja ambapo watu hawatakimbilia kwenye kutafuta ubunge, kwani maisha ya haki ndio yatakayokuwepo. Mungu hamfichi mnafiki.
 
Safi well said mkuu. Takrima zianze kuchunguzwa.
 
Back
Top Bottom